Kitu gani kimefanya Vodacom wadharau agizo la Serikali kuhusu bei za bando?

Kitu gani kimefanya Vodacom wadharau agizo la Serikali kuhusu bei za bando?

Vifurushi vimeanza kupanda hata JPM hajawa raisi. Naona umeanza kutumia simu 2020.
Kulikuwa na night bando karibia makampuni yote, voda walishusha mpaka ikawa 4GB kwa 1500 na mwenzake Tigo.
Mwaka jana 2020 mwezi wa 10 vifurushi vya night bando Halotel na Airtel speed vilikuwa kama konokono.
Mwaka jana 2020 vifurushi vya tigo vilikuwa moto.
JPM huyu huyu ambaye ameshindwa hata kuajiri hata kutoa nyongeza ya mshahara. Nimkumbuke?
Bora hata ameondoka maana alikuwa anaenda kuigawa nchi
Hapo ndiyo mtamkumbuka R.I.P. John Pombe Magufuli. Ninyi wenyewe mlishangilia serkali kutoingilia uhuru wetu. Kampuni kama VODA inachukuliwa kama mtu, na ina haki kuwerka bei ya bidhaa yake kama inavyoona inafaa. Sasa mnang'aka! Sasa kinachotembea ni nguvu ya pesa. Naona Mbowe mbele akiwa na mchakato wa kuishtaki VODA! Kazi iko.
 
Hata angekuwepo angefurahi sana maana angeona ndiyo muda muafaka wa watu kutokuwepo mtandaoni maana wasingepata muda wa kumfuatilia Kigogo.
Angekuwa ana roho nzuri angeifungia Twitter? TTCL yenyewe ilimshinda. Tutamkumbuka kwa lipi?
Alikufa mafuta ya kupikia rita 5 yalikuwa yanauzwa kwa shilingi ngapi vile?
Hapo ndiyo mtamkumbuka R.I.P. John Pombe Magufuli. Ninyi wenyewe mlishangilia serkali kutoingilia uhuru wetu. Kampuni kama VODA inachukuliwa kama mtu, na ina haki kuwerka bei ya bidhaa yake kama inavyoona inafaa. Sasa mnang'aka! Sasa kinachotembea ni nguvu ya pesa. Naona Mbowe mbele akiwa na mchakato wa kuishtaki VODA! Kazi iko.
 
Unakumbuka wakat cement inapanda bei mwanzoni mwa oct mwaka Jana? Badae serekali ilikuja kutoa tamko kuwa vifaa vya ujenzi ikiwemo cemnt zishuke bei na zirudi bei ya awali lakin wala hazijashuka Hadi leo huku nilipo tunanunua 21,500/= mfuko mmoja wa cemnt

Mimi nilicho gundua ni kuwa viongoz wameshatuona wa Tz ni mabwege wakija kwetu wanakuja na sura nyingine na wakienda kwa hao wawekezaji wanaenda kwa sura zingine, mchawi mkubwa hapa ni kodi tu, na viongozi wanapo jidai kutoa matamko huwa ni matamko ya kinafki yalio jaaa uongo mtupu, nyuma ya pazia wao ndiyo waumizaji wakubwa wa raia
 
Sasa si muwahame?

Yaani mnailalamikia Voda utadhani ni watoa huduma za simu/data pekee...
 
Ni siku ya kumi sasa tangu vodacom wapandishe bei za vifurushi vya matumizi ya simu. Baada ya malalamiko ya wateja, serikali kupitia TCRA walitoa tamko la kutaka makampuni yote yarudishe bei za zamani wakati suala hilo likishughulikiwa. Pia na rais Samia S Hassan naye akakazia kwa kutaka suala hilo la upandishaji holela wa vifurushi lisijirudie tena. Baadhi ya makampuni ya simu ikiwemo Hallotel walitii agizo hilo na kurudisha bei za mwanzo. Lakini sijui ni kwa kiburi au dharau, vodacom mpaka leo wamekaidi agizo hilo na kuendelea na bei zao mpya ambazo kwa hakika ziko juu mno.
Hivi hawa jamaa nani anawalinda kiasi cha kukaidi hata agizo la rais? Je TCRA au waziri husika mbona nanyi mko kimya?
Wenye share Vodacom Tanzania wanajuna na serikali
 
Bei ya zamani unaijua? Usikute zile unazoita za zamani ilikuwa ni promotion tu aliamua Vodacom kibiashara ila hizi za sasa labda ndio bei za zamani.
 
Back
Top Bottom