Kitu gani kinachonisumbua?

Kitu gani kinachonisumbua?

sverige

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
417
Reaction score
176
Sijui kama Niko sawa wakuu naombeni Ushauri kabla ya kwenda hospital kwasababu siko sawa. Kama mwezi mmoja uliopita nilishikwa na tonses pamoja na homa kali sana, nilitumia dawa haikuchukua wiki moja nikawa nimeuona.

Cha kusikitisha ikawa bado nasikia maumivu kwambali pale ninapokula chakula kigumu Na huwa ninakohoa sana pamoja na kutema makohozi kwa wingi. Nikaona ni jambo la kawaida. Sasa jana ndio nikajiangalia kujua ni nini kinachonisumbua kufungua mdomo nikakuta kilimi changu kimeshikana na kugandana na upande mmoja wa tezi ya kushoto na kuna usaa kwa mbali.

Naombeni msaada kuhusu hili tatizo langu, je ni nini hasa?
 
Kweli umeona vitu hivyo vyote bado huendi hospitali tu?

Ingekuwa zamani tungesema ni kimeo, miaka hii hakuna tena hicho kitu.
 
Wahi Hosptal mkuu Dr atakukagua vizuri na kujua apime nini hii mitandao ni nyongeza tu ya maisha.
 
Kweli umeona vitu hivyo vyote bado huendi hospitali tu?

Ingekuwa zamani tungesema ni kimeo, miaka hii hakuna tena hicho kitu.

Mamndenyi kwani siku hizi kimeo kimeenda wapi? manake zamani kidogo tu wanasema kakate kimeo tena kwa witch-doctor
 
Kweli umeona vitu hivyo vyote bado huendi hospitali tu?

Ingekuwa zamani tungesema ni kimeo, miaka hii hakuna tena hicho kitu.

Nitaenda hospital mkuu lakini kabla yoyote naamini hapa pia Kuna wataalam
 
Jamani nataka kujua huu ugonjwa niwakawaida? Mzizimkavu nawengine njooni mnipe msaada nimekuwa nawasiwasi sana
 
itakuwa tonsilitis. maambukizi kwenye tonsils. tonsils huvimba na unakuta kimeo nacho kimekuwa laini kuliko kawaida. siyo ishu sana nenda hospitali wakupe dawa. kama vipi tafuta azithromycin lakini ni vema uende hospitali.
 
Jamani nataka kujua huu ugonjwa niwakawaida? Mzizimkavu nawengine njooni mnipe msaada nimekuwa nawasiwasi sana
Via kwanzaafya.blogspot, pole sana utakuwa unasumbuliwa na vidonda vya koo au ugonjwa wa GERD ambavyo ni matokeo ya vidonda au fangasi mdomoni kwa muda mrefu hivyo wahi hospitali mapema kwani maambukizi yanaweza kusambaa kwa kasi asa kuelekea kwenye ubongo na uti wa mgongo.
 
Back
Top Bottom