Kitu Gani ulihisi unakijua lakini badae ukagundua kumbe ulikuwa hujui chochote

Kitu Gani ulihisi unakijua lakini badae ukagundua kumbe ulikuwa hujui chochote

Kihonda Kanisani

Senior Member
Joined
Sep 1, 2024
Posts
144
Reaction score
523
Ni hivii zamani nilikua najua jenereta /Generator ni kifaa kinachofua umeme au tuseme ni kifaa kinachobadili nishati ya mwendo kuwa nishati ya umeme.

NIliamini hakuna jenereta inayoweza kufanya kazi ya kuzalisha umeme bila kupewa nishati ya mafuta ( petrol au diseli). Nilikuwa najua jenereta iliiweze kufanya kazi lazima liungurume. Ili kuzalisha umeme. Lahaulah nilikuwa mbali na ukweli.

Ukweli ni huu, mafuta au muungurumo wala si sehemu ya jenereta wala haina uhusiano wowote na jenereta. Ile injini inayounguruma sio sehemu ya jenereta. Jenereta inabadili nishati ya mwendo kuwa umeme ile injini na kelele zake sio sehemu ya jenereta . Umeme unatakiwa kuzalishwa kwa kuzungusha shafti inayozungusha coili zilizokuwa katikati ya usumaku. Na hiyo ndio jenereta lenyewe au tuseme jenereta ni shafti inayozungusha coili iliyo katika mfumo wa sakiti katika ya usumaku.

Sasa kipi kizungushe shafti?
Baadhi ya jenereta zimetengenezwa shafti zake zinazungushwa na mjongeo wa juu na chini wa pistoni katika piston silinda kwa kuchoma nishati ya mafuta ,mfano jenereta zinazotumia petrol na disel.

Jenereta zingine zimetengenezwa shafti zake zinazungushwa na turbine/tabaini . Generatos hizi hazipigi kelele lakini zinabadili nishati ya mwendo kuwa umeme. mfano genereta zinazopatikana Kidatu na mtera.

Jenereta nyingine shafti yake inazungushwa na binadamu kupitia tairi. Mfano jiko la baiskeli ( dainamo) kwa baiskeli za zamani iliwekwa katika tairi ya nyuma . Ukifyatua kichwa cha shati kinagusa tairi na mzunguko wa shafti utategemea na mzunguko wa tairi ukiongeza na umeme unsongezeka na taa inawaka zaidi.

Ilinichukua miaka mingi kuelewa kuwa jiko la baiskeli(dainamo) nalo ni jenereta . Wakati nilijua jenereta lazima lipige kelele.

Shea kitu kimoja ulichohisi unajua kwa muda mrefu kumbe ulikuwa mweupe kabisa

Muwe na maandalizi mema ya pasaka.
 
Nilijua sisiemu ni wapumbavu kumbe🙄🙄🙄..kumbe ni wapumbavu walio tukuka
 
Back
Top Bottom