Kitu gani ulikipenda ukiwa Mtoto

Kitu gani ulikipenda ukiwa Mtoto

Nilipenda sana kuratibu na kusimamia ndondi.
mimi ndio nilikuwa refa wa ngumi,yaani muda wa kutoka shule wanafunzi wenzangu walikuwa wanakuja kuniuliza kama kuna pambano.Yaani walikuwa wakitibuana tu,wanakuja kwangu kutoa taarifa nami nawaingiza kwenye ratiba.Wakati mwingine nilikuwa naratibu mapambano mpaka matatu kwa siku.Sheria ilikuwa ukitoka damu basi pambano limeisha na wewe uliyetoka damu ndio umeshapigwa.Kimbembe ni siku siri ilipovuja kwa walimu baada ya mtoto mmoja kula kichapo mpaka jino likatoka na mzazi akaja kesho yake shule.Yaani nilipomuona tu kijana yuko na mzazi wake wanaenda ofisi ya mwalimu mkuu,nilikula kona na sikutokea shule wiki nzima.Nilikua nikitoka nyumbani naaga naenda shule kumbe naishi porini.Bahati mbaya kuna siku dogo mmoja aliniona nimebana miembeni,daaah akaenda kumtonya ticha.Asikuambie mtu,darasa zima lilitumwa kunikamata,kuna watu wana mbio sio mchezo.Nilichezea fimbo sana siku hiyo na ndio nikastaafu rasmi urefa na kuratibu ndondi.
Dah! Waalimu wakaua kipaji chako cha urefa.
 
Mi nilikuwa napenda ile mnakusanya mchanga then mnaweka mti juu kisha taratiiibu mnaanza kupunguza mchanga huku mnaimba tule wali tumbakishie baba sasa ole wako uangushe kile kijiti na wakudake kabla hujashika mti wa ukomboz utajuuta
 
1480670_10208518289144024_630956384189674884_n.jpg

Mimi nilipenda Ukuti ukuti wa mnazi wa mwisho akamatwe atiwe gerezaaaaaaani....

we ulipenda mchezo gani zaidi
 
Back
Top Bottom