Kitu gani ulishawai poteza au ibiwa ambacho kwako kilikuwa na thamani kubwa...

Niliwahi kuibiwa begi la laptop lenye laptop,kamera,bahasha yenye vyeti vyote vya taaluma kuanzia Sekondari hadi chuo kikuu,cheti cha kuzaliwa,hati ya kiwanja n.k, wallet na hela zake kidogo pamoja na vitambulisho vyote na kadi za benki. Huwa naamini ningekuwa na moyo mwepesi ningekufa kwa mstuko siku ile. Niliumia sana ila Mungu ni Mkuu daima niliibiwa January 2014 nikapigiwa simu na polisi niende nikavifate central police mwezi November mwaka huohuo.
 
Niliibiwa wallet ikiwa na €700 ilikua ya matumizi ufaransa ***** siwezi sahau tena wafanyakazi wa Airport ndo waliniambia.
 
Dah...kisu changu Cha kukunja...nikiwa darasa la 4...kinaniuma sana[emoji41]
 
Simu yangu ya kwanza kumiliki motorola ilikua ilala,wazee wa finger walinichomolea aisee
 
Nilipambana kununua PC ikaibiwa na mtu niliyekuwa naishi naye
mimi nilipotezewa na jamaa yangu nikabaki na charger yake/kitabu cha maelezo na risiti yaani huwa naviona inaniuma sana maana niliinunua laki 5 kipindi hicho.
 
Kuibiwa kusikie tu kwa jirani...nilibiwa simu ya kichina niliyonunua 70,000 mwaka 2009...kipindi hicho ndo kwanza zinaingia walikata nyavu dirisha wakasepa nayo..niliumia sana aisee...

Mara ya pili wamevunja home wakabeba flat screen samsung 32" na laptop ya samsung pia hiyo ilikuwa Jan 1 2015...siku hiyo nilipagawa sana hata sikulala....

2016..wakaja tena wakabeba..flat TLC 32" na laptop pb....safar hii sikupagawa nikachukulia kama changamoto tu...
Ila nimekoma kununua flatsecreen za gharama...
 
Pole ikawaje mkuu
 
Pole sana mkuu
 
Enhe ninkweli at
 
Mwaka 2016 nilifika Mwanza nikakaribishwa na wazee wa kazi....waliniibia simu 2, laptop,vyeti vyote, mkufu wa dhahabu, mapochi na kila kitu....waliniachia nguo tuu...niliumia sana ilikuwa karibisha mgeni
 
Kuku wangu
 
Dah! Huwa naikumbuka gari yangu moja niliyoinunua kwa Milioni ishirini na mbili, na ndani ya mwezi mmoja ikawa Scrapper! It was fucken so painful. Unajua milioni 22 ni sawa na tofali elfu ishirini... Hizo pesa ningekuwa nimeshajengea hata shule. Since then, niliuza magari yoote yaliyobakia sasa ni mwendo wa dala dala tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…