Kuna siku nilikuwa natoka kwenye mihangaiko yangu. Sasa kufika maeneo ya njia panda ya Mwenge nikawa navuka barabara. Wakati navuka, kuna jamaa naye akawa anavuka in opposite direction (tukawa tunaangaliana).
Sasa tukawa kama tunataka kupamiana. Maana nikienda kushoto, jamaa nae anaenda kushoto. Nikienda kulia, jamaa nae anaenda kulia, hadi tukawa tumekaribiana kabisa. Nikaganda kidogo ili kumruhusu yeye afanye uhamuzi, then tupishane, jamaa nae akawa kama vile ananisikilizia Mimi ndo nifanye uhamuzi. Haya yote yalitokea kwa haraka sana, ndani ya muda mfupi, na muda huo kuna cruiser ipo speed inatokea uelekeo wa Kawe inakuja uelekeo wetu Mimi na yule jamaa maana tupo katikati ya barabara, na muda huo zimeruhusiwa gari zinazotoka upande wa Kawe kwenda makumbusho na zinazokata Kona kwenda mawasiliano, za kutokea Makumbusho zimepigwa pini.
Baada ya kuona yule jamaa nae kasimama hanipishi, nikaamua kupita kushoto kwake, ili yeye apite kulia, cha ajabu na yeye akaja upande ule ule, tukawa tumekaribiana kabisa. Baada ya kuhisi hapa tutagongwa na Ile cruiser kwa uzembe, nilijikusanya nguvu zangu zote, nikaamua kumpiga push yule jamaa ili wote tuangukie upande wake, maana sikuwa tena na namna.
Ajabu ni kwamba nilivyojipeleka kumpush, nilijikuta napush hewa, alaf nikaangukia upande wa pili, yule jamaa hakuwepo aisee. Kile kitendo cha kuanguka, Ile cruiser ilipita speed, ikanikosa kidogo sana na haikusimama Wala kupunguza mwendo. Watu waliokuwa maeneo Yale walijua nijirusha kukwepa Ile cruiser, kumbe Mimi nilikuwa nataka kumpush mtu, na wao hawakuona mtu yoyote.