Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Umeniambia nisearch miss corridor alafu sasahivi unaniambia sielewi??[emoji23][emoji23][emoji23] Kwahiyo natakiwa nisearch miss high heels???

Bado nimekosa haya nitumie wewe hiyo link nisome...

Alafu mbona maswali yangu unayakwepa???

Umesema wazungu hawaamini uchawi nimekutumia juu story zao mpaka na movie unajifanya huoni???
 
mkuu unajichanganya sana, vitabu vinavyo zungumzia juu ya uwepo wa muumba vinataja pia uwepo wa uchawi wewe unasema vina makosa (unabagua hili sawa hili hapana)

ukwel uchawi upo
Sema kitabu Gani nikuambie makosa yake. Vitabu hivyo hivyo vinasema dunia ni flat, juu Kuna ceiling ambayo inashikilia maji ya mvua, mbinguni ni mawinguni, popo ni ndege, sungura anacheua, nyoka na punda wanaongea, magonjwa yanasababishwa na mapepo(sio bacteria), jua linazunguka dunia na linaweza kusimama au kurudi nyuma etc . Ni uwongo. So kuamini hivi vitabu automatically unaweza amini chochote kile ndo maana unaamini uchawi
 
Siye alikuwa anatikisa kitanda[emoji3]

Sent from my itel W5002 using JamiiForums mobile app
 
Nimekuambiaje hata wazungu ambao hawajaelimika pia wapo.

 
Ingine nilishuhudia Tunduma border..Mkongomani ameibiwa dagaa....akakodisha gari la matangazo akazunguka mji mzima anatangazia watu walioiba dagaa wawarudishe...mwisho akaenda uwanjani...akavua koti akalirusha juu...MKWARA...koti likabaki hewani....kama dk 45huku akipiga mkwara kwamba koti likianguka chini basi waliomwibia dagaa hawatapona......dagaa wote walirudi
 
Kuna siku nmeenda car wash nimeosha gari yangu vizuri sana nikarudi nikapaki home nikaenda nikalala ..Asubuhi natoka kwenda kazini nafungua mlango wa gari nakuta kipande Cha mkaa kwenye siti ..sikuwahi kuelewa ule mkaa uligikaje ndani ya gari ..ila mwamba aliyeniuzia gari alikuwa anateseka sana hata ukaribu uliisha ..mwishoe niliuza nikaagiza Moja Kwa Moja .
 
🤣🤣Mi Sina Imani, we ndo una Imani. Imani ni kubelieve kitu bila uthibitisho ni kama wewe na uchawi. Ungeleta uthibitisho wa uchawi hapa mbona ningekuwa freshi tu. Ushaskia mi nasema jua halipo au mbwa hawapo au miti haipo
Ndo maana nimekwambia haya Mambo yapo kiroho zaidi kama unataka uyaone nenda kiroho zaidi utayaona na utashangaa acha kujichekesha hapa.
 
Again, hallucinations na wivu wa mafanikio. Tafuta elimu facha kazi, acha kuwaza maujinga.
HUNA UNALO LIJUA ISIPOKUA UJINGA NDO UMEKUJAA TU KICHWANI TAFUTA MARIFA, KIJANA UJIONEE ULIMWENGU UNAVYO ENDA KUNA MAMBO MENGI KWENYE HII DUNIA YANAJIENDESHA KIUCHAWI!! HATA HAO WANA SAYANSI UNAO WAMINI HUWA WANASHINDWA KUYATAMBUA MAMBO YA KIUCHAWI, mfano mzuri ni ndege ya aina ya Pan American flight 914 ilyopotea miaka 37 badae kurudi Duniani hapo Wana sayansi walishindwa kupata jibu hiyo ndege ilipotelea wapi,, yapo mambo mengi yanayothibitisha uchawi na hao wanasayansi WANASHINDWA kupata majibu yake wanabaki kimya,,
punguza ubishi tafuta marifa then ingia kiroho zaidi utayaona huwez Pinga kitu ambacho hujakiona wakati huo wewe unaishi kimwili na vitu vyenyewe vipo kiroho, so nakushauri ishi kiroho usipo yaona njoo hapa ubishe
 
Miaka ile pale Ludewa mawengi walitengeneza umeme wa maji. Walitengeneza vizuri sana na ulikuwa unawaka vizuri tuu. Sasa kimbembe alialikwa JK kuja ķufungua huo mradi eeenh bwana eenhh. Siku km saba hivi kabla mgeni hajafika JK kila wakitest mitambo haiwaki ng'ooo. Jaribu jaribu na wewe ng'odo hamna kitu. Wataalamu walidata hatari maana mgeni rasmi siku zinasogea na kitu anachokuja kufungua kibovu hatari pia ni rais wa nchi. Sijui ilikuwaje mmoja wa wataalum akawa analalamika kwa mama ntilie pale barabarani karibu na mahakama. Kuwa walitengeneza vizuri mtambo ulikuwa unapeleka umeme huko lakini sasa hauwaki. Watu wakamwambia nenda kwa mzee fulani pale kijijini mkazungumze nae maana walikuwa wamekasirika kutowashirikisha. Basi yule mtaalum katoka pale mkuku mpk kwa yule mzee akamuelezea project yoote na kwanini imekwama kwa sasa. Yule mzee akauliza kwanini mnatengezea umeme sisi mnaruka hapa mnapeleka huko misheni wakati sisi tunapata shida hapa. Wakajieleza pale kuwa ule umeme ni kidogo ila serikali italeta project kubwa kila mtu atapata. Yule mzee akasema kumbe aaah haya nendeni mkawashe hamna shida. Kurudi kuwasha ngoma imekubali mashine imewaka na kesho yake ndiyo JK akaja aisee. Nikasema watu wameroga mpk machuma hii hatari.
 
That is a burden proof.
siwezi thibitisha kitu ambacho hakipo wewe unayesema kipo unapaswa thibitisha. Hivi unaelewa hilo?
Wapi nimekwambia uthibitishe kitu ambacho hakipo?

Point yangu ni kwamba unapinga uchawi pasina kutoa sababu za msingi yani kwa sababu hauamini tu uchawi basi, na kibaya zaidi hata huo uchawi wenyewe hata hauelewi vizuri ila unatumia nguvu kuupinga.
 
siku nyengine ukikuta wamevunja Nazi.... okota... osha... tafuna....
 
kuna watu wa kuitwa Wavidunda hao.... Morogoro hukooo... wanaishi juu milimani udzungwa... pembeni ya Bwawa la Umeme Kidatu! Jamaa walizuia Mradi wa Ujengaji wa Bwawa... mpk Nyerere akaingilia kati.... Mpk leo Jamaa wanashushwa kutoka Milimani kwa Magari ya TANESCO kila Alhamis kwenda Mnadani na Jioni wanarudishwa bureeee! Uchawi upo!
 
Twende taratibu, kwahiyo wote wasio fanikiwa ni kwa sababu hawana commitment discipline na consistencny na kwamba wote waliyofanikiwa wana hizo sifa?
 
Wapi nimekwambia uthibitishe kitu ambacho hakipo?

Point yangu ni kwamba unapinga uchawi pasina kutoa sababu za msingi yani kwa sababu hauamini tu uchawi basi, na kibaya zaidi hata huo uchawi wenyewe hata hauelewi vizuri ila unatumia nguvu kuupinga.
Unaelewa maana ya burden proof?
Siwezi thibitisha kitu ambacho hakipo kwani mbona hivi vitu ni vyepesi
Wewe umesema watu wanafanikiwa kwa uchawi ni KAZI YAKO uthibitishe na si mimi.

Mpaka sasa hujathibitisha kama mtu anafanikiwa kwa uchawi ILA mimi nimekuonyesha watu waliofanikiwa kwa kufanya KAZI.

Thibitisha hoja yako.
 
Twende taratibu, kwahiyo wote wasio fanikiwa ni kwa sababu hawana commitment discipline na consistencny na kwamba wote waliyofanikiwa wana hizo sifa?

Tunaweza tumia reference za watu ILI tujue huyo mtu alikuwa consistency, discipline na akaji commit na bado akashindwa fanikiwa kwenye carrier yake?

Nionyeshe celebrity hawa Kati ya messi na ronaldo kafanikiwa kwa uchawi?
Mafanikio yana level. But eventually wote hao wanafanya kazi na zinaonekana

Nadhani ulisema uchawi ni kutumia dawa asili au mitishamba kudhuru kama sikosei

Kwa sentensi hiyo nataka unipe connection na mtu kufanikiwa.

Kama mimi naweza kuelezea nikinywa panadol kichwa kinapoa na nitakupa connection.
Shida yako unakosa kutetea hoja yako kwa kuiundia uhusiano na unachodai.

Mpaka sasa hujathibitisha.
 
Mi nikisema Nina range Rover si utauliza liko wapi. Coz the burden of proof ipo kwangu. Sasa mi nikianza kusema unajuaje mi Sina, unaweza dhibitisha kwamba Sina and the lyk...🤣 naonekana mjinga. Ndo wewe Sasa. Ukisema uchawi upo prove it
Nikikwambia kuwa wewe hauna range rover kisha nikamalizia kwa kusema siwezi kuthibitisha visivyokuwepo ila nikasisitiza kuwa hauna range rover, hapo utasemaje?
 
Nikikwambia kuwa wewe hauna range rover kisha nikamalizia kwa kusema siwezi kuthibitisha visivyokuwepo ila nikasisitiza kuwa hauna range rover, hapo utasemaje?

Huwezi thibitisha vipi kuna kampuni ipo inazalisha range rover tayari contradiction.
Ukimwambia hana range rover ina maana the burden of proof ipo kwake si kazi yako kuthibisha ni yeye aliyesema anayo range rover unaelewa lakini mkuu?

Thibitisha hoja yako ya mtu kufanikiwa kwa uchawi bado unazunguka mpaka sasa.
 
Explain in details Sasa with verifying evidence sio story za mtaani na kijiweni
Wewe unadai hakuna kabisa uchawi na chuma ulete ni katika aina za uchawi unaozungumziwa sana tu, sasa elezea hiko kinachoitwa chuma ulete kuwa si kweli kwamba ni uchawi kama inavyoaminika. Tumie hiyo elimu yako kunieleza mie nisiokuwa na elimu kwamba ni vp huko watu(wasio na elimu) kuona kupotea kwa hela na kuhusisha na uchawi kuwa si uchawi bali ni nini hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…