Kitu kinachoshindikana kwenye kizazi cha "Gen Z" ni Ndoa tu

Ejolisi

Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
57
Reaction score
87
Kwanza kikazi chetu ni kizuri kinaleta changamoto kwenye jamii na kuonyesha ma "gap" mengi ambayo hayajazibwa vizuri kwenye jamii.

Kinapima uwezo na utoshelevu wa malezi yenu (Millennials) Je, yanaweza kutumika katika nyakati tofauti tofauti maisha yakiwa yaendelea kubadilika kila siku.

Gen Z au watoto wa 90s na 2000s ukiangalia vizuri kinachotushinda ni mahusiano tu. Sasa nyie wahenga angalieni tatizo ni nini? Sio kutusema tu haisaidii.

Na suluhu ziwe applicable sio mnaongelea vitu haviwezekaniki ooh unajua zamani ilikuwa hivi, tuko sasa hivi hatuko zamani

Na hata hawa vijana wa kataa ndoa sio wakulaumiwa ni kwamba hawaoni maana toeni maana.

Pia soma:
 
Kuzaa ni muhimu, ila ndoa kwa sheria za sasa ni mtego mzito
 
Endeleeni kukataa ndoa na tukutane finali uzeeni ndo mtajua! Sasa hivi tianeni mimba na kusepa! Mdada ukishatiwa mimba kusuka au kunyoa ni juu yako kwasababu wanaume hawataki kwaoa kutokana na mojawapo ya sababu nyie ni wasumbufu na si waaminifu wakati wanaume hawataki kuwajibika kama baba!
 
Tatizo hakuna wanawake mabikra ndo maana ndoa zimekuwa ngumu.
 
Naona watu kama mnachanganya mambo, hicho kizazi cha Gen- Z kipo Kenya, Tanzania na Uganda hakipo, tusijiweke kwenye kundi tusilostahili.

Vijana wa Kenya wametuonesha wengine kwa vitendo nini tukiamua tunaweza kufanya, ni wakati wetu sasa wa kuamka nasi tufanye kama wao ili tu qualify kuitwa Gen -Z.

Wale viumbe wamepmbana na mafisadi ya nchi yao bila msaada wa Raila baba yao, wamemwambia baba pumzika nyumbani tuchie sisi hii kazi tuimalize wenyewe, naa wameimaliza vizuri serikali ya Ruto imenyoosha mikono, huku kwetu bila Mbowe, Lissu, Mdude na Mwabukusi hakuna tunachoweza...

Tuamke sasa.
 
Huu ni ukweli mtu.
Hiyo generation Z ipo Kenya, Tz hakuna kitu.
 
Imenyooshaje mkono juu nawakati financia bill a.k.a budget imepita japokua kulikuwa na maandamano acha ushabiki
 
Imenyooshaje mkono juu nawakati financia bill a.k.a budget imepita japokua kulikuwa na maandamano acha ushabiki
Wakati wakenya jana usiku wako barabarani wakishangilia serikali yao kusalimu amri, wewe sijui ulikuwa wapi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…