DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Katika kipindi hiki ambacho bajeti imeanza kujadiliwa bungeni, ni vyema kutathmini majukumu ya serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo na jinsi ambavyo wanasiasa wanahusika katika mabadiliko yoyote yanayofanyika nchini.
Nime bahatika kuangalia mikutano ya hivi karibuni ambapo wabunge wamekuwa wakijadili mambo mbalimbali na mawaziri. Majadiliano hayo yaliishia hatua ambayo wabunge walihoji mara kwa mara kuhusu mipango ya "Serikali" kukamilisha miradi mbali mbali kwenye majimbo yao. Kwa wabunge wote wa Tanzania, nani ni "Serikali?". Kama wawakilishi wa wananchi bungeni, jambo lipi linawazuia wao kuwa na maamuzi ya kutosha ya kuwawezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye majimbo yao?
Katika kutathmini majukumu ya serikali, Je wizara zimezidiwa? Kama kweli zimezidiwa, inawezekana kwamba watu wa juu tu ndio wanahusika zaidi katika kuhakikisha kwamba miradi inafanyika ipasavyo na cha muhimu zaidi kuliko vyote ni usimamizi wa fedha. Uaminifu wa kutosha ni muhimu katika kuhakikisha kwamba majukumu ya serikali yana gawanywa kwa wahusika wote kulingana na ngazi ya uongozi.