Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kuna vitu vingi ambavyo wanaume vinawakera ili mara nyingi hawawezi kuvisema kwa wake zao na wakisema wanajua vinaleta ugomvi tu. Kati ya hivyo vingi vitatu ni vikubwa. Naomba nitaje hiki cha tatu na sijui labda dada zetu watabadilika.. (uwezekano wa hilo ni sifuri!)
Usiku wa manane.. mmelala mtu anaanza "Baba Chanja... unajua mama mdogo hatujamuona siku nyingi kweli kwanini tusiende kumtembelea weekend hii". Yaani hiyo ni saa tisa za usiku mtu kakosa usingizi anaamua kukuamsha na wewe wakati labda ulikuwa kwenye dili zako ndotoni..
Hivi ni lazima kweli mtu aanza kuzungumza mambo mazito usiku wa manane utadhani kuna emergency.?
Kama hukai na mke/mwanamke ndani hili huwezi kulielewa...