Kitu rahisi kuliko vyote dunia ni kulalamika

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Posts
4,446
Reaction score
8,215
Habari wakuu, nimefanya utafiti mdogo nimegundua kitu rahisi kuliko vyote dunia ni kulalamika. Asilimia kubwa ya watu wanaopenda kulalamika huishia kuwa masikini, na ndio maana umasikini ni synonym ya kulalamika. Na pia nimegundua kitu kigumu zaidi duniani ni kuwajibika. Kuwajibika na kutimiza ndoto zako uwe mwenye mafanikio ni ngumu sana.

Na ndio maana ni ngumu sana for instance Tanzania kumkuta mtu kama Bakhresa, Reginald Mengi, Ghalib Said Mohammed (GSM), Mohamed Dewji(Mo Dewji), Yusuf Manji kulalamika. Ukimkuta mtu aliyefanikiwa akilalamika basi ujue huyo angekua masikini basi pangechimbika.

Watu wanapenda sana kulalamika Ili ionekane kwamba matatizo na changamoto wanazopitia vimesababishwa na wengine. Na ndio maana watu wengi sana especially vijana, mitandaoni wanalaumu serikali/wanasiasa as if ni chanzo cha matatizo yao. Chunguza sana hapa JF asilimia kubwa ya nyuzi zinazofunguliwa hapa ni za kuilaumu serikali na wanasisa ( Kwa sasa mambo ya DP is the name of the game watu full kulaumu). Why watu wanalumu hawachukui hatua hata hao akina Samia waondolewe madarakani. Halafu inakuja kufika 2025 wanaume hata hawagombei hata huo urais na kumwachia Samia awe Rais ili waje wamlaumu baadae. Kwa nini tunapenda kulaumu hatuchukui hatua kwa vitendo?

Watu waliofanikiwa hawapendi kulaumu laumu hovyo hovyo, mfano. Mo Dewji alivyotekwa kwa muda mrefu but alivyoachiliwa sikuona akiilaumu serikali,ccm au mtu yoyote. Yusuf Manji alivyonyanyaswa na akina Magufuli pamoja na Makonda lakini sijawahi muona akilalamika na kulialia hovyo, kumbuka jamaa aliwekwa ndani mpaka akaota mandevu Kama beberu but the guy is still going strong. Hata huyu Bakhresa sijawahi msikia akilalamika TFF kuzipendelea timu za kariakoo huku timu yake ya Azam Sports ikifanyiwa fitna.

Nitakupa mifano miwili tu ambayo utagundua watanzania wanapenda sana kulalamika ila hawapendi kujiwajibisha wao binafsi

Sakata la mwanafunzi wa shule ya Sekondari Panda Hill aliyetoroka shuleni aitwaye Ester Noah Mwanyilu, kuonyesha watanzania tunapenda sana kulaumu, aliporuhusiwa aongee akaanza kwa kusema "naomba serikali imchukulie hatua mwalimu Jimmy". Akaulizwa achukuliwe hatua kwa sababu gani? Lakini binti akakaa kimya. Huyu binti hakutaka kuzungumzia kabisa makosa yake ya kutoroka shule, ku cheat kwenye mtihani, kwenda kulala na wanaume akina baba Jose na wala hakutaka kuomba msamaha kwa wazazi wake pamoja na watanzania kwa ujumla kwa kuibua taharuki. Hajataka kuwajibika ila yeye ameona alaumu wengine ili yeye aepukane na aibu na fedheha aliyoisababisha mwenyewe. Na pale kwenye conference ameonekana yeye ni innocent kabisa. Kwa hiyo kwake yeye hoja kubwa pale ya kuijadili ni mwalimu kuchukuliwa hatua.

Sakata la DP World watu wanalumu tu lakini hawachukui hatua ya kwenda kwenye maandamano, watu ni wachache sana waliojitokeza kwenye maandamano lakini kwenye kulaumu ni wengi sana. Kwa mfano najiuliza ni nani hapa JF alikuwepo kwenye maandamano, hivi akina Mshana watakua walikuwepo kweli????, Mwanamke alikuwepo mmoja tu let say ni Evelyn Salt HAYA wanawake wengine mbona wanalaumu tu hawchukui hatua yoyote???

KULAUMU NI KAZI RAHISI SANA KULIKO KAZI ZOTE DUNIANI
 
Na hasa kwetu ngozi nyeusi,,Huko Marekani wamebobea haya mambo, Leo hii ile Black Lives Matter ishafilisika, wahusika walikuwa wanalipana mabilioni kindugu ndugu.

Waafrika wa huku kwetu wakienda huko wanafanikiwa zaidi.
 
Huu ni ujinga mwingine, wewe ni msemaji wa nani hadi mpangwe?mazuzu ni watu wa kulalama humu huku mikia yao ikiwa Imekatwa
Mkuu watu wamepagaw kila mtu wanamlalamikia.... Lawana kibao utafikir tupo mahakaman
 
Na hasa kwetu ngozi nyeusi,,Huko Marekani wamebobea haya mambo, Leo hii ile Black Lives Matter ishafilisika, wahusika walikuwa wanalipana mabilioni kindugu ndugu.

Waafrika wa huku kwetu wakienda huko wanafanikiwa zaidi.
Ngoz nyeus ni lawana tu sisi hatuwez ku solve matatizo
 
Habari wakuu, nimefanya utafiti mdogo nimegundua kitu rahisi kuliko vyote dunia ni kulalamika. Asilimia kubwa ya watu wanaopenda kulalamika huishia kuwa masikini, na ndio maana umasikini ni synonym ya kulalamika. Na pia nimegundua kitu kigumu zaidi duniani ni kuwajibika. Kuwajibika na kutimiza ndoto zako uwe mwenye mafanikio ni ngumu sana.

Na ndio maana ni ngumu sana for instance Tanzania kumkuta mtu kama Bakhresa, Reginald Mengi, Ghalib Said Mohammed (GSM), Mohamed Dewji(Mo Dewji), Yusuf Manji kulalamika. Ukimkuta mtu aliyefanikiwa akilalamika basi ujue huyo angekua masikini basi pangechimbika.

Watu wanapenda sana kulalamika Ili ionekane kwamba matatizo na changamoto wanazopitia vimesababishwa na wengine. Na ndio maana watu wengi sana especially vijana, mitandaoni wanalaumu serikali/wanasiasa as if ni chanzo cha matatizo yao. Chunguza sana hapa JF asilimia kubwa ya nyuzi zinazofunguliwa hapa ni za kuilaumu serikali na wanasisa ( Kwa sasa mambo ya DP is the name of the game watu full kulaumu). Why watu wanalumu hawachukui hatua hata hao akina Samia waondolewe madarakani. Halafu inakuja kufika 2025 wanaume hata hawagombei hata huo urais na kumwachia Samia awe Rais ili waje wamlaumu baadae. Kwa nini tunapenda kulaumu hatuchukui hatua kwa vitendo?

Watu waliofanikiwa hawapendi kulaumu laumu hovyo hovyo, mfano. Mo Dewji alivyotekwa kwa muda mrefu but alivyoachiliwa sikuona akiilaumu serikali,ccm au mtu yoyote. Yusuf Manji alivyonyanyaswa na akina Magufuli pamoja na Makonda lakini sijawahi muona akilalamika na kulialia hovyo, kumbuka jamaa aliwekwa ndani mpaka akaota mandevu Kama beberu but the guy is still going strong. Hata huyu Bakhresa sijawahi msikia akilalamika TFF kuzipendelea timu za kariakoo huku timu yake ya Azam Sports ikifanyiwa fitna.

Nitakupa mifano miwili tu ambayo utagundua watanzania wanapenda sana kulalamika ila hawapendi kujiwajibisha wao binafsi

Sakata la mwanafunzi wa shule ya Sekondari Panda Hill aliyetoroka shuleni aitwaye Ester Noah Mwanyilu, kuonyesha watanzania tunapenda sana kulaumu, aliporuhusiwa aongee akaanza kwa kusema "naomba serikali imchukulie hatua mwalimu Jimmy". Akaulizwa achukuliwe hatua kwa sababu gani? Lakini binti akakaa kimya. Huyu binti hakutaka kuzungumzia kabisa makosa yake ya kutoroka shule, ku cheat kwenye mtihani, kwenda kulala na wanaume akina baba Jose na wala hakutaka kuomba msamaha kwa wazazi wake pamoja na watanzania kwa ujumla kwa kuibua taharuki. Hajataka kuwajibika ila yeye ameona alaumu wengine ili yeye aepukane na aibu na fedheha aliyoisababisha mwenyewe. Na pale kwenye conference ameonekana yeye ni innocent kabisa. Kwa hiyo kwake yeye hoja kubwa pale ya kuijadili ni mwalimu kuchukuliwa hatua.

Sakata la DP World watu wanalumu tu lakini hawachukui hatua ya kwenda kwenye maandamano, watu ni wachache sana waliojitokeza kwenye maandamano lakini kwenye kulaumu ni wengi sana. Kwa mfano najiuliza ni nani hapa JF alikuwepo kwenye maandamano, hivi akina Mshana watakua walikuwepo kweli????, Mwanamke alikuwepo mmoja tu let say ni Evelyn Salt HAYA wanawake wengine mbona wanalaumu tu hawchukui hatua yoyote???

KULAUMU NI KAZI RAHISI SANA KULIKO KAZI ZOTE DUNIANI
Umesema ukweli mkuu, hata huku kwenye ndoa wanaume tunalaumiwa hatuwaridhishi wakati wao style wanayoita ni kifo cha mende na wakilala kama gogo, shahidi To yeye huyu hapa
 
Umeingia chaka kwenye utafiti wako!

Dangote aliwahi kulalamika kuhusu mazingira ya uwekezaji Tz.

Mara nyingi wenye hela hawalalamiki hadharani hizi nchi zetu sababu ya mirija yao itakatwa ila malalamiko wanayo.
 
Back
Top Bottom