Kituko:Baada ya Yanga kukodi daladala jana

athury92

New Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
2
Reaction score
4
Kitendo cha Yanga kukodi daladala kama usafiri wao kutoka uwanja wa ndege Mwanza kimezua gumzo kwenye vyomba vya habari na mtandaoni

Klabu ya Yanga tayari imewasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya pambano lake la Jumamosi dhidi ya Mwadui FC, na ule wa Jumatano dhidi ya Stend United.

Yanga ambao wanaongozwa na tajiri mkubwa mwenye asili ya kihindi Yusuph Manji, imeondoka Dar es Salaam alfajiri ya leo kwa usafiri wa ndege kupitia Mwanza na kisha kupanda basi la kukodi hadi Shinyanga.

Kituko kikubwa ambacho kimewakuta mabingwa hao ni kupanda Daladala aina ya ‘Hiece’ tatu kutoka uwanja wa ndege Mwanza hadi Hotelini na baadaye kukodisha basi kubwa ambalo liliwapeleka hadi mkoani Shiyanga na kuwasili majira ya saa tatu asubuhi.

“Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desidediti ameiambia Goal, waliamua kukodi Hiece hizo, baada ya basi walilokuwa wamelikodi kuchelewa kufika uwanja wa ndege na ndipo walipokodi daldala hizo ili kuepuka wachezaji wao wasikae kwa muda mrefu uwanja wa ndege,” amesema Baraka.

Yanga imesafiri na kikosi chake kamili kwa ajili ya michezo hiyo miwili na kocha wake Hans van der Pluijm, amekuwa na matumaini makubwa kuhakikisha wanarudi Dar es Salaam na pointi zote sita.

1474003469464.jpg
 
Yanga wakimataifa leo hii kwenye daladala , ama kweli
 
Nyumba ya jirani kunaungua
Walianza kusema, Manji atajiuzulu.... Ghafla kimya!

Sasa Yanga kupanda Daladala, wanasema Manji kawanyima pesa!

Mwaka huu sijui mtamsingizia nani kama mkikosa Ubingwa na Yanga akabeba.
 
Kitendo cha Yanga kukodi daladala kama usafiri wao kutoka uwanja wa ndege Mwanza kimezua gumzo kwenye vyomba vya habari na mtandaoni

Klabu ya Yanga tayari imewasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya pambano lake la Jumamosi dhidi ya Mwadui FC, na ule wa Jumatano dhidi ya Stend United.

Yanga ambao wanaongozwa na tajiri mkubwa mwenye asili ya kihindi Yusuph Manji, imeondoka Dar es Salaam alfajiri ya leo kwa usafiri wa ndege kupitia Mwanza na kisha kupanda basi la kukodi hadi Shinyanga.

Kituko kikubwa ambacho kimewakuta mabingwa hao ni kupanda Daladala aina ya ‘Hiece’ tatu kutoka uwanja wa ndege Mwanza hadi Hotelini na baadaye kukodisha basi kubwa ambalo liliwapeleka hadi mkoani Shiyanga na kuwasili majira ya saa tatu asubuhi.

“Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desidediti ameiambia Goal, waliamua kukodi Hiece hizo, baada ya basi walilokuwa wamelikodi kuchelewa kufika uwanja wa ndege na ndipo walipokodi daldala hizo ili kuepuka wachezaji wao wasikae kwa muda mrefu uwanja wa ndege,” amesema Baraka.

Yanga imesafiri na kikosi chake kamili kwa ajili ya michezo hiyo miwili na kocha wake Hans van der Pluijm, amekuwa na matumaini makubwa kuhakikisha wanarudi Dar es Salaam na pointi zote sita.

View attachment 401213
Mbona Mikia fc walikodi Coastar from DSM to Songea!
 
Mateso kwa zamu. Simba msimu uliopita walikodi daladala hiace pia kwenda uwanjani majimaji songea
 
Sasa hiyo salam
Subirini mkimkopesha huyo muhindi anawafirisi mtabaki na majengo
 
Back
Top Bottom