athury92
New Member
- Sep 13, 2016
- 2
- 4
Kitendo cha Yanga kukodi daladala kama usafiri wao kutoka uwanja wa ndege Mwanza kimezua gumzo kwenye vyomba vya habari na mtandaoni
Klabu ya Yanga tayari imewasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya pambano lake la Jumamosi dhidi ya Mwadui FC, na ule wa Jumatano dhidi ya Stend United.
Yanga ambao wanaongozwa na tajiri mkubwa mwenye asili ya kihindi Yusuph Manji, imeondoka Dar es Salaam alfajiri ya leo kwa usafiri wa ndege kupitia Mwanza na kisha kupanda basi la kukodi hadi Shinyanga.
Kituko kikubwa ambacho kimewakuta mabingwa hao ni kupanda Daladala aina ya ‘Hiece’ tatu kutoka uwanja wa ndege Mwanza hadi Hotelini na baadaye kukodisha basi kubwa ambalo liliwapeleka hadi mkoani Shiyanga na kuwasili majira ya saa tatu asubuhi.
“Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Desidediti ameiambia Goal, waliamua kukodi Hiece hizo, baada ya basi walilokuwa wamelikodi kuchelewa kufika uwanja wa ndege na ndipo walipokodi daldala hizo ili kuepuka wachezaji wao wasikae kwa muda mrefu uwanja wa ndege,” amesema Baraka.
Yanga imesafiri na kikosi chake kamili kwa ajili ya michezo hiyo miwili na kocha wake Hans van der Pluijm, amekuwa na matumaini makubwa kuhakikisha wanarudi Dar es Salaam na pointi zote sita.