Kituko cha bibi / babu yako unachokikumbuka.

Simara

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
7,512
Reaction score
23,925
Leo nimekumbuka vituko vya babu yangu, Babu yangu alikua anapenda sana kujifungia chumbani kwa hiyo muda mwingine unampelekea chakula huko huko ! Siku hiyo nimeenda nampelekea chakula naita babu babu kimya wakati namuona ndani kakaa nikaita tena babu akanijibu babuka yani nilicheka nusu nizimie sijui alikuwa na hasira gani hahahaha!!

Kuna siku kagoma kulala eti kilipo kitanda sio kila siku kinapokua so wamrudishie kinapokaa, sasa wanamuuliza huwa kinakaa wapi anaonyesha sehemu lilipo kabati la nguo. ha ha ha ha nilicheka ile siku maana aligoma kulala kama hawataki ni heri alale chini kesho arudi kijijini!! ikabidi kitanda kifunguliwe wasogeze kabati wakifunge tena.....wakina anko na mama walinunaa kwa hasira!!!

Share kituko chohote cha bibi/ babu yako unachokikumbuka
 
Mie bibi yangu miaka hiyo akiwa hai aliwahi kuja Arusha kile kipindi cha baridi si unajua tena baridi yake inavyokuwa, yaani usiku akitaka kulala mbali na blanket na shuka mpaka umewekee na vimkaa kwenye jiko uvunguni kwa muda kwanza ili apate lile joto ndio anakubali kulala. Na bila kumuwekea halali aisee na hata akilala atasononeka huyooo.

Uzuri kitanda kilikuwa kirefu hivyo ikawa ni lazima kufanyiwa hivyo japokuwa kulikua na hatari ila hakukuwa na jinsi si unajua tena mtu akiwa mzee anakuwa kama mtoto vile.
 
Mie bibi yangu miaka hiyo akiwa hai aliwahi kuja Arusha si unajua tena baridi yake, yaani usiku akitaka kulala mbali na blanket na shuka mpaka umewekee na vimkaa kwenye jiko uvunguni ili apate lile joto ndio analala. Na bila kumuwekea halali aisee na hata akilala atasononeka huyooo.

Uzuri kitanda kilikuwa kirefu hivyo ikawa ni lazima kufanyiwa hivyo japokuwa kulikua na hatari ila hakukuwa na jinsi si unajua tena mtu akiwa mzee anakuwa kama mtoto vile.
ni hatari kweli mlikua mnauacha hadi asubuhi?
 
Babu yangu akiwa amelewa gwagwa/pombe ya ndizi alipenda kujigamba kijiji kizima ati yeye ndo kasomesha wanae.wananzengo /wanakijiji wakakasirika mmoja akamwotea mvua imenyesha akamkata panga.japo alimjeruhi tu hakufa.japo sasa amelala.alikuwa mwenyewe mpaka la 12 enzi hizo.
 
Babu yangu ni mfugaji ana ng'ombe nyingi sana,sasa ni kama amekua affected psychologically kwamba kila mtu huwa anam_treat kama ng'ombe

Sasa kuna mtoto wake mmoja(dingi yangu mdogo) alikua mtoro sana wa shule,siku moja Babu akaona huyu dogo asintanie,akavizia asubuhi kabisa jamaa bado kalala akamkamata akamfunga kamba za kufungia ng'ombe na akaanza kumswaga kama anaswaga ng'ombe hadi skuli huku akimtandika fimbo dingi mdogo

kufika skuli wanafunzi ndo wako paredi afu jamaa ndo analetwa huku amefungwa kamba na babu
Ilikua noma sana siku hiyo wanafunzi na walimu walicheka sana siku hiyo
 
Baada ya kuvunja ungo tu nikiwa kidato cha pili, bibi yangu nilipokuwa nikitoka shule (nilisoma day) alinikagua bikira au popote pale mradi nimeenda kitaa nikirudi nilikaguliwa vua pichu lala kitandani panua miguu isipokuwa siku za damu tu zinginezo hilo zoezi lilifanyika, hasira nilokuwa naipata basi tu,
Alale mahali pema bibi
 
Looh maskin
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baada ya kuvunja ungo tu nikiwa kidato cha pili, bibi yangu nilipokuwa nikitoka shule (nilisoma day) alinikagua bikira au popote pale mradi nimeenda kitaa nikirudi nilikaguliwa vua pichu lala kitandani panua miguu isipokuwa siku za damu tu zinginezo hilo zoezi lilifanyika, hasira nilokuwa naipata basi tu,
Alale mahali pema bibi
Sikupatii picha hasira yake[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom