Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Nilipokuwa mtoto nilikuwa napenda sana wali maharage na hata iweje ni lazima mimi nipikiwe Chakula hicho.Siku moja hali ikawa ndivyo sivyo nyumbani na bi Mkubwa akaniambia bwana mzee leo hakuna wali utakula ugali tuu jioni. Nikajifanya mimi bingwa wa hasira si nikanyea unga uliokuwa umehifadhiwa kwenye kindoo.Kilichonipata ni Mungu tu anajua.
Ulikula ile mixture ya unga na udiko...
 
="miss chagga, post: 15239698, member: 148879"]kaolewana anagongwa na wengine ha ha ahhaha
Hahaha..yaani nilitunzia raia mkuu... Da, Jah atanilipa au pengine ashanilipa sacrifice yangu..
 
Mara ya kwanza kabisa kwenda town kwa sistaangu (ila siyo huyu atoto wala Heaven Sent , hawa wa juzi juzi tu wananifuata mimi kwa mbali huko) ndo kukukuta chai ktk maisha yangu, tulizoea kunywa uji tu home kijijini. Basi nikawa nimeipenda sana ile chai ya rangi na ule ushamba wangu wa kijijini. Nakumbuka siku hiyo sista yuko huko uani anafua fua, mi nikaingia zangu ndani taratibu hadi kabatini nikatoa chupa ya chai tulikuwa wenyewe tunaita semosi. Nia yangu niibe chai angalau pafu kidogo, basi kufika nikaifungua ile semosi fasta nikafungua mdogo fasta tupia huko chai weeeeeeeeee niliunguaaaaa mbaya mdomoni, nilishuhudia natema vinyama tu kwa jinsi nilivoungua na chai. Sijui kwanini sikuwaza kuwa ni ya moto, yaani sina jibu zaidi ya utoto!!
Hahaha atoto nakufaa huku mbavu zanguuuuu. Basi usijali ntakuwa nakuandalia chai kila ukija
 
Hii thread imenifanya nijue JF members wengi wamekulia vijijini.
 
mimi nakumbuka nikiwa darasa la tatu niliku mpenzi sana wa samaki sasa mzee alikuwa kila week analeta samaki wa bichi mama anawakaanga fresh anatia ndani ya jokofu.. mimi hata unipe samaki mzima kiu hamu haishi .. nikawa na katabia cha kuokoa samaki nakula upande mmoja halafu namgeuza anaonekana ajaguswa wakati wa kupika mama akiuliza kila mtu anakataa.. siku moja jioni jioni nikafanya huo mchezo wangu wa udokozi acha mfupa unipalie kooni mama ndiyo akagundua mwizi wake ni nani kipigo nilichopata baada ya kutolewa mfupa aisee mpaka leo siwezi gusa kitu cha mtu bila kuomba,........... udokozi mbaya hasa wa samaki
Hahaaaaa dah!!!
 
Nikiwa mdogo niliwahi kuiba hirizi iliyokuwa inapumua ya mzee mmoja mchawi aliyekuwa anaogopeka sana pale kijijini. .kwenda kuipasua nilikuta kinyonga aliyekatwa mkia alitweta kwa kukosa pumzi vizuri
Lile tukio lilikuwa kubwa na baya pale kijijini mpaka ikibidi nihamishwe
Mkuu kumbe haya mambo ulianza mapema eeh, no wonder......
 
Mimi nilijipaka utomvu wa majani flani kule kwetu mamndenyi kwenye uume - wakaka wakubwa walitudanganya inaongeza ukubwa wa uume - niliumwaaaaaaaaaaa...lakini ilisaidia nilitahiriwa kabla ya kufikia umri wa kutahiriwa (kwa mila zetu).

Kumbe mbinu za kutaka kuongeza ukubwa wa "kifaa" zinaanza toka utotoni eeeh!!
 
Nakumbuka i was7, alafu wakati huo ndio nimejua kuogelea basi natamani kuogelea kila wakati na vyanzo vya maji viko mbali.

Siku nikaondoka mchana jua kalii kwenda kisimani kuchota maji maana mchana wengi huwa hawaendi coz of jua.
Kufika nikaangalia kushoto na kulia hakuna mtu nikavua nguo nikatumbukia kuogelea.
Aisee nilipitiliza nikanywa maji ya kutosha, nikiwa ktk hali ya kutapatapa akatokea mama(kama bahati tu) akaniokoa na kunitapisha maji yote.
Akaniuliza imekuwaje? Nikamjibu niliteleza, akauliza uliteleza vipi ikiwa nguo umevua ziko pembeni? Nikabaki natoa macho tu, akanipa stik za kutosha, daaah!!
 
Back
Top Bottom