Kituko cha utotoni ambacho sitakisahau

Teh teh teeeeh! Ukataka kumbikiri sister! Ila sijui kuna nguvu gani kwenye maneno mabaya, watoto huwa rahisi sana kuyadaka.
Teh teh..Ukisikia kitu kipya unakidaka fasta...
 
Nimecheka sana! Hiyo tabia alikuwa nayo rafiki yangu, kuna siku alidandia kwenye tela la tractor, kumbe ule mlango haukuwa na lock, sasa kakimbizia weee hadi akalifikia, ile kushika tu ule mlango ukashuka na kutua kichwani! Alilazwa hospitali wiki za kutosha!
 
Teh teh..Ukisikia kitu kipya unakidaka fasta...
Nakumbuka watoto wa my sister wanefuatana wa kike na wa kiume(wa kiume ndio mkubwa)

Kuna siku vilikwenda kucheza hivyo vikachelewa kuoga, mama yao akawachapa kisha akawaogesha usiku sebuleni saa2 wakati tukiwa tunakula.

Akaanza kuogeshwa mdogo wa kike alivyamaliza akaenda kumwaga maji na kuweka mengine sasa yule mdogo akachukua maji kidogo ya baridi akammwagia kaka yale kidogo mgongoni kaka mtu akastuka na kwa hasira akamtusi mdogo wake "nitaku*fira" aisee tulistuka dada kidogo azimie, sijui alilisikia wapi tusi hilo, alikula makofi hadi tukamtetea.
 
Teh teh..Hiyo kali aisee...Maskini ya Mungu utakuta hapo hata hakajui kanamaanisha nn...Pata picha ndo anasema hivyo mbele za wageni
 
Ha haa unakuta maza mnoko kuliko mzee,afu akianza kumpampu mzee utatamani ukimbilie hata barabarani aise
Yaani mie baba hakuwahi hata kunifinya na nilikuwa kipenzi chake, ila mama daaaah!! Yaani nikikumbuka vipigo na nilivyokuwaga chautundu hata havihesabiki, unakula stiki hadi unajiuliza "huyu kweli mama yangu"
 
ha ha ha ha ha...
duh hii kali
 
Teh teh..Hiyo kali aisee...Maskini ya Mungu utakuta hapo hata hakajui kanamaanisha nn...Pata picha ndo anasema hivyo mbele za wageni
Unadhani hata maana kalikuwa kanajua basi, kalijiropokea tu sijui alilisikia wapi nae akalidaka, duuuuh yaani tulibaki kimyaaa tunatoa macho tu.
 


Hahahah...mkuu nimependa sana kisa chako!

Ila zaidi ya yote nimependa uandishi wako mwandiko umezingatia hatua zote za kiuandishi muundo na maana nukta, koma na kila herufi umeiumba ipasavyo.

Kama ungekua mwalimu ungebarikiwa zaidi kwa kuwasaidia wengi miandiko yao humu na huko ulipo.
 
Ahsante mfilipino mwenzangu teh.
 

Hirizi hiyo alikua anaitundika nyumbani? Nawaza uliibaje.
 
Hahaha...ushaanza kunifanya nasmile smile hapaa...

Ile ya mishumaa kwenye mvua huitaki tena eeeh...
Hahaha basi usismile bana

Teh ile idea wengi watakuwa washacopy bana, nitafutie kitu kingine cha uhakika bana
 
Yaani mie baba hakuwahi hata kunifinya na nilikuwa kipenzi chake, ila mama daaaah!! Yaani nikikumbuka vipigo na nilivyokuwaga chautundu hata havihesabiki, unakula stiki hadi unajiuliza "huyu kweli mama yangu"
He hee mama ni anapiga mpaka unaomba poo. Nilikua naangusha kilio cha nguvu nalia weee kama nusu saa hivi mpaka anakuja kunibembeleza mwenyewe ndio nanyamaza.

Kwenye hii michezo ya kujipikilisha nilichezea vifinyo na vichapo mana kila siku nilikua naiba vitu ndani tunaenda kujipikilisha kwenye njeka.
 
Ngoja nisome zoooote. Huenda nikakuta aliefanya kituko kama nilichofanya.
 
Mie navituko vingi sanaa maana utotoni nilikua mtundu kupindukia
1. Nikiwa na pacha wangu tunatengeneza magari ya mbao gafla bandani kulikua na kuku kaatamia akaanza kupiga kelele tukamcharanga na majembe na kupasua mayai yake ila baba alivyorudi toka kazini akaishia kupigwa na butwaa tu hatukuchezea kichapo.
2. Nikiwa kwa bibi angu, kuna baba angu mdogo alikuja na coins kibao kwa ajili ya biashara zake akaziweka chumban kwa bibi ambako mie nilikua nalala. Nikawa naiba zile coins nanua mapulizo na watu pale mtaani wakawa wananituma naenda nawachukulia maana nilikua hamna nachoelewa ila kuna siku akanifuma nilichezea bakora za kutosha.
3.nikiwa darasa la kwanza la pili nilikua sipendi shule..nikawa nasumbua sana ila darasani nilikua vzuri coz nilikua sipendi kua kilaza...sasa io siku nilichelewa namba nikagoma kwenda shule mama akanitolea uvivu akanibeba msobe msobe na fimbo mkononi dah nikatupa viatu njiani sweta begi ila mama hakuniacha hadi kwa head teacher wakaitwa vijana wa darasa la saba wakanishika mikono na miguu nikachezea bakora za kutosha dah ila nashukuru mungu nilimalza salama had kufika hapa nilipo
 
Hahaha basi usismile bana

Teh ile idea wengi watakuwa washacopy bana, nitafutie kitu kingine cha uhakika bana


Hahah...kweli ile itakua imeshaibwa

Mfilipino vuta subira niwaze tupate amazing nyingine tena kwa valentine day inabidi iwe ni amazing plus
 
Hahah...kweli ile itakua imeshaibwa

Mfilipino vuta subira niwaze tupate amazing nyingine tena kwa valentine day inabidi iwe ni amazing plus
Poa poa, nakuaminia mfilipino mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…