Roho mbaya hiyo sista, looh
Heaven Sent ana roho ya huruma ya kuzaliwa ndoa maana ananipa pole ya utundu wangu wa utotoni
BTW hivi hawa watoto wa siku hizi nao wanafanya vitu amazing kama hivi vya enzi zetu? am just curious
Hahaha mtoto ni mtoto tu. My lil sis yeye alikuwa anaonja kitu chochote mbele yake. Yani kila anachokiona anabugia tu fasta. Tushapata kesi kibao na yeye kwa mzee maana mara leo anywe mafuta ya taa, kesho kabugia mseto dawa, mara atake kuonja mafuta ya betri yani ni heka heka tu. Si unawajua wazee mlivyo, nyie mnaona tu kama sisi hatupo makini na mtoto, wazembe
Siku ya siku, bi mkubwa alihisi kuna panya kaingia ndani. So akamtegea dawa, kosa ni kwamba alichukua kipande cha samaki kizuri tu kwa matumizi ya binadamu, akapaka dawa akategesha kwenye kisosi. Ameingia bafuni kuoga, anatoka kipande cha samaki hakipo. Mmh machale kumcheza haiwezekani dk chache panya awe ashabeba samaki wote yule, kamuita dogo, kumuuliza uliingia chumbani dogo kagoma. Maza kampa kofi takatifu ikabidi kaseme kenyewe ndo kamechukua samaki Hahaha. Mama presha Tafuta maziwa fasta, kumpigia simu mzee fasta (ilikuwa weekend uzuri) wakamuwahisha hospital. Kufika hospital ikaonekana dawa haina nguvu kihivyo so wakampa tu nini sijui
Tatizo sasa mzee wangu ni anapenda utani, me sioni ndani. Ile hospital aloenda ndo huwa tunatibiwa hapo mara nyingi so doctors tumezoeana nao. Dr mmoja akaanza kumzingua mzee " eti daah ila mshkaji hiki si kiashiria kizuri, haiwezekani mtoto achukue hadi samaki wa panya, home lazima kuna uhaba wa nyama nyama. uwe unawanunulia nyama watoto bana", mzee akaishia tu kucheka.
Usiku tumekaa mzee akaanza kuniambia "daah ila watoto wanatiaga aibu jamani, huyu dogo kanifedhehesha leo, utadhani nyama halagi, kumbe anakula hadi basi", nilichekaje