Kituko cha Zaire kwenye 1974 FIFA World cup

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Mwishoni mwa miaka ya 1960 Mobutu aliwekeza sana kwenye mpira wa miguu kwa lengo kwamba nchi yake iweke record ya kuingia fainali za kombe la dunia, miongoni mwa aliyoyafanya ni kutafuta wachezaji na kuwapa nyumba mpya na magari aina ya VOLKSWAGEN ilipofika mnamo mwaka 1974 Zaire ilikuwa nchi ya kwanza ya sub sahara Africa kushiriki kombe la Dunia, lakini kuna bwana mmoja anaitwa MWEPU ILUNGA alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Zaire (the leopards) wakati ikicheza na Brazil alifanya kituko kilichowaacha mdomo wazi wazungu

jamaa wakati wa faulo (sio mpenzi wa mpira hivo sina uhakika na hili jina) wenzie wakiwa wameweka defence yeye alienda akapiga mpira wakati sio team yake ilipaswa kupiga mpira

“he ran out of his team's defensive wall and kicked away a free kick before the ball was in play.”

Zaire hata hivo ilishindwa hii match kwa 3–0. pia walifungwa mechi zao mbili za mwanzo walipocheza na Scotland 2–0 na Yugoslavia 9–0.


kitendo hiki kilimvunja moyo Mobutu akaacha na kufadhili mpira akajikita zaidi kwenye muziki (wasanii walipewa state sponsorship )
Waliporudi Zaire walipokelewa na bus ya jeshi (kawaida walikuwa wakipokelewa na bus za kifahari) ikawapeleka Ikulu walipomkuta Mobutu ana hasira akawauliza “kwahiyo mlidhani mtagoma ? siku nyingine nitawatupa wote jela,nimewapa magari na nyumba kila mmoja wenu alafu mmefanya haya ?”

baada ya hapo Mobutu aliwapiga marufuku kusafiri,majina na picha zao yaliwekwa kila Airport na bandarini yakiwa na ujumbe uliosomeka HAWARUHUSIWI KUONDOKA NCHINI ili wasiende kucheza mpira ulaya maana timu za ulaya ziliwataka, baadae wachezaji waliishi maisha ya umasikini wa kutupwa na wengine walifariki wakiwa masikini kutokana na kosa walilofanya


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah aliwakatili Sana wachezaji,kwann awazuie kusafiri nje? So sad
alichukia kuona pesa yake na muda wake umeenda bure, so akaona ni kama wamemfanyia jeuri akawakomesha hivo,walikosa kazi na kuwa ma dereva taxi
 
Wana bahati maana miaka 16 baadae kuna mchezaji wa Colombia aliuawa kwa kupigwa risasi na shabiki kwa kosa la uwanjani,,
Kuweka kumbukumbu sawa Miaka 20 baadae Andres Escobar wa Colombia aliuwawa na wakamaria baada ya kujifunga kwenye fainali za Kombe la Dunia pale Marekani
 
Kuweka kumbukumbu sawa Miaka 20 baadae Andres Escobar wa Colombia aliuwawa na wakamaria baada ya kujifunga kwenye fainali za Kombe la Dunia pale Marekani
Yes, kutoka 1974 hadi 1994 ni miaka 20.Wakamaria walimfuata home kwake wakamtandika shaba wakapotea kusikojulikana. Escobar alijifunga kwa bahati mbaya
 
Yes, kutoka 1974 hadi 1994 ni miaka 20.Wakamaria walimfuata home kwake wakamtandika shaba wakapotea kusikojulikana. Escobar alijifunga kwa bahati mbaya
Ni home kwake? Mbona kuna sehemu nilisoma alikuwa anatoka disco wakamfata parking akijiandaa kuondoka na gari lake
 
Ni home kwake? Mbona kuna sehemu nilisoma alikuwa anatoka disco wakamfata parking akijiandaa kuondoka na gari

Ni home kwake? Mbona kuna sehemu nilisoma alikuwa anatoka disco wakamfata parking akijiandaa kuondoka na gari lake
Wakati ule walitangaza kwamba alitandikwa nje ya nyumba yake, sasa siku hizi tuna access ya kupata taarifa sahihi zaidi so unalosema inawezekana kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…