Kituko gani ulichokifanya ukiwa shule

Nakumbuka nilipokuwa O level kuna manzi Fulani nilikuwa namkubali sana mtoto mzuri kinoma.
Siku moja tuko tunapata Lunch (boarding)akapita akiwa na wenzake kwa mbali dah nilishtukia nimesimama na kumuita kwa Sauti Kubwa Mara kadhaa( genye mbaya sana) bahati mbaya kumbe kaongizana na matron halafu shule ilikuwa seminary.
Kilichitokea baada ya hapo siri yangu
 
Nikiwa darasa la tano Oysterbay Primary School kipindi hiko Mwalimu Mkuu akiwa Marehemu Mama Ng'ambi ( R.I.P ) huku kukiwa na Walimu wawili wanoko sana ambao kwa bahati nzuri wote walikuwa wametoka JKT ( namaanisha ile JKT ya enzi hizo siyo hii yenu ya nyoro nyoro / mayai mayai ya sasa ) akina Mwalimu Nyagabona na Mwalimu Bahati aliyekuwa mwana Familia ( nadhani Mkewe mdogo ) Jaji Augustino Ramadhani Mimi na Mwenzangu mmoja tuliacha historia ambayo najua hata Dada yangu Brendah Msangi aliyepo sasa hapo CCBRT Msasani ( kama Bosi wao ) akikumbuka atacheka mno kwani nilikuwa nikimsumbua na kumuudhi sana wakati tunasoma hapo.

Kutokana na ' utundu ' wetu Mimi na mwenzangu ambaye nae ni mdogo wake Kiundugu kabisa na Joseph Kusaga wa Clouds Media Group mwenye jina linaloanzia na herufi ' W ' tulijulikana sana kwa kuwa Watundu na Watukutu pale Shuleni na kama kuna Wanafunzi kwa ile miaka yetu ambao walikuwa Viboko vya Kutukuka basi ilikuwa ni Mimi na Rafiki yangu mkubwa kabisa ' W ' hivyo tulikuwa na tabia ya kutegea ule Ukaguzi wa kila asubuhi kabla ya kuingia darasani na kukimbilia kwenda kujificha katika Pori moja ambalo sasa kumejengwa Ukuta wa Taasisi moja Nyeti na Hatari hapa Tanzania ambayo nimeibatiza jina la ' Eagle Wing House ' kisha tukishahisi Gwaride lile la asubuhi limeisha basi tunarudi zetu darasani na kuendelea na maisha yetu.

Nakumbuka siku moja kama kawaida yetu tulienda kujificha pale pale na siku hiyo kwa bahati mbaya sana kuna ' Wanako / Kaa ' fulani wakawa wamekuja na Mbwa wao ambao walikuwa ni wakali kweli kweli ambao muda mwingi walikuwa wanatiririka na wanaserereka eneo lile lile tulilozea Mimi na mwenzangu ' W ' kujificha na bahati mbaya pamoja na uchakaramu / utundu wetu wote tulikuwa ni waoga sana na Mbwa hivyo ikatubidi tubadili mbinu ya kukwepa lile Gwaride la asubuhi.

Baada ya kuona kwamba kule Porini kumebuma tuliamua sasa taratibu kabisa tena kwa minyato kurudi eneo la Shule na kutafuta darasa moja ambalo kwa juu lina sehemu ya uwazi ( darini ) ambapo tulilipata hivyo Mimi na cha Utundu mwenzangu ' W ' tukapanda na kwenda kujificha kule juu huku nje Wanafunzi wenzetu wakiendelea na Gwaride na kwa mbali tukimsikia Mwalimu mnoko / kaa Nyagabona akitembeza ' bakora ' zake za Kutukuka kama kawaida kwa wale ambao walikuwa na makosa mbalimbali.

Kumbe wakati ule Sisi tumeingia mule darasani kujificha darini kuna mmoja wa Kiranja alituona tukiingia na nakumbuka alikuwa na ' Bifu ' sana na Sisi kwakuwa tulikuwa tukipinga nae ule mchezo wa ' Kuputa ' na kumpiga Mtu ' teke ' akiwa amebong'oa ( Watu wa zamani mtanielewa kwani huu mchezo mmeucheza sana ) hivyo huyu Kiranja alikuwa na bahati mbaya sana na Sisi kwani mara nyingi sana tulikuwa tukimputa Yeye kitu chochote kitamu kitamu alichokuwa ameshika na akijisahau na akiinama basi tulikuwa tunampiga sana ' mateke ' kama tulivyokubaliana nae katika mkataba wetu usio rasmi na wa hatari pia kwa afya ya Binadamu na usiompendeza hata Mwenyezi Mungu pia.

Sasa huyu Kiranja ' adui ' yetu alipotuona tu Mimi na ' W ' tumetega Gwaride na kuingia mule darasani kujificha darini haraka mno akaenda kuwatonya hao Walimu wawili Nyagabona na Bahati hivyo wakaamu na wao kutuwekea mtego kabambe pale pale ambapo walichokifanya sasa wala hawakutufuata pale pale bali walituchunia na kuendelea na Gwaride pale Uwanjani na walichofanya sasa ni kwamba wale Wanafunzi waliokuwa wakilitumia lile darasa hawakurudishwa mule na wakawekwa mahala kwanza huku wakipewa Kazi ili Sisi ' Watukutu ' tuje sasa tutegwe vizuri.

Kumbe kwa ' Upumbavu / Upopoma ' wetu Sisi tukadhani labda mambo yamekuwa safi na kama kawaida yetu hawa Walimu wetu wawili na ambao kiukweli walikuwa wakitutafuta sana Mwalimu Nyagabona na Mwalimu Bahati tukaanza kujipa matumaini kule kule juu darini kuwa mambo sasa mukede na dukinaa. Wakati ' Mapopoma ' sisi kule darini tukijiachia kumbe huku chini darasani wakawa wamekuja hawa Walimu wawili na wamejificha chini ya Madawati bila Sisi kujua.

Ndipo sasa Mimi na mwenzangu ' W ' tukaamua kushuka / kuteremka kutoka kule darini ambapo nakumbuka alianza ' W ' na hatimaye Mimi nikafuata ambapo wakati tunashuka tulikuwa tunawachamba na kuwabeza mno kwa maneno hawa hawa Walimu wanoko / kaa wawili pasipo kujua kwamba wamo mule mule darasani wamejificha. Tulipomaliza tu kushuka na kujifutafuta vumbi na kutaka sasa kutoka mara ghafla tukawaona Walimu hawa wawili wakiibuka na pale pale ' manunda mapopoma ' tukakamatwa.

Baada ya hapo ninachokumbuka tu ni kwamba Kwanza tulichezea ' bakora ' za kutosha kutoka kwa hawa Walimu wawili kisha tukapelekwa Ofisi ya Walimu ambako na kwenyewe pia tulichezea ' bakora ' za kutosha na nakumbuka kuna Mwalimu wangu mmoja wa darasa jina limenitoka nae pia akakumbushia kwamba ana Kesi na Mimi kwa kuwa nilikuwa mwizi sana wa Peni za Watu na ' Makompasi ' na tabia ya kuwategeshea Kioo Wanawake halafu nawachungulia ' Mbunye ' zao hivyo na hapo tena nikala ' bakora ' za Kufa Mtu na mwisho tukapelekwa kwa Mwalimu Mkuu Marehemu Mama Ng'ambi ambaye nae alitupa zake ( namaanisha bakora ) kisha pale pale Wazazi wetu Mimi na ' W ' ambaye nakumbuka Kipindi hiko Baba yake alikuwa ni Bosi Mkuu wa Shirika la KIUTA hivyo wakaja wote wawili na kuitishwa ' school baraza ' la dharura.

Jamani katika maisha yangu yote sikuwahi kupigwa ' Kipigo ' kile na Mzazi wangu kama ambacho nilipigwa pale mbele ya Wanafunzi na nakumbuka hawa Wazazi wetu wote wawili Kwanza kila mmoja alimchapa Mwanae kisha baadae Baba yangu na Baba yake ' W ' nao wakapeana ' Kolabo na kufanya Mashap kama la Coke Studio ' la ' kutuchapa ' ambapo sasa hatukuishia tu kuchapwa bakora bali sasa tulipigwa ngumi na mateke na bahati mbaya Wetu wote hao walikuwa ni wana ' Medani ' tulipigwa nusura ya Kuuliwa ndipo Walimu wakatutetea na kusalimika na tukaonywa na kuomba msamaha kwa Wanafunzi we wenzetu na yakaisha.

Mimi nikadhani kwamba labda mambo yote yale yaliishia pale pale Shuleni kumbe pale ilikuwa ni ' demo ' tu na nilipofika Nyumbani sasa Baba GENTAMYCINE akanionyesha sasa rasmi kwamba hakupitia huko katika Vikosi vya ' Kimedani ' bure na ki bahati mbaya ambapo ile naingia tu Nyumbani nikakaribishwa kwa kupewa Jembe, Kolea na Fyekeo na kupelekwa katika Bustani moja hivi pale home ambayo ina udongo mgumu na Nyasi nyingi ili nilime na nifyeke huku akinisimamia na nakumbuka kama siyo Marehemu Bibi yangu kuwepo Kipindi kile pale Nyumbani basi yawezekana kwa Kichapo na adhabu ile basi leo hii nisingekuwa Binadamu hivi na sasa ningekuwa Marehemu tayari. Bibi aliingilia kati na kumkataza Mwanae ' Mdingi / Mshua ' kuwa aniache na kweli nikasalimika ila nakumbuka baada ya hapo nilikaa home kama wiki mbili hivi kwa Kuugua na Kuuguza majeraha ya ' Kipondo ' cha mseto / pamoja kutoka kwa Walimu na Wazazi.

Tokea siku hiyo hadi leo hii GENTAMYCINE nilibadilika sana na kuwa Mtoto mwema, mtulivu na mkemea maovu ya aina yoyote ile. Na ndiyo maana tokea siku hiyo hadi leo hiii nikiona tu Mwanafunzi yoyote yule ama mtukutu au mtoro huwa nakuwa mwepesi kumuita na kumshauri kuwa asiwe hivyo na kuna ambao nimekuwa nikiwaona wanafanya mambo ya ' hovyo hovyo ' huwa nawachapa / nawapiga ' bakora ' hadharani au nawabeba mzobe mzobe hadi Kwao kwa Wazazi / Walezi wao na nawashtakia kwani sitaki na wao yawakumbe yale yaliyotukuka Mimi na ' W ' mwaka 1990. Akhsanteni sana Walimu wangu na Wazazi wangu kwani mliniinyoosha kweli na bila nyie japo mlikuwa kweli Wanoko / Kaa sidhani kama leo hii ningekuwa hivi na mbarikiwe nyote na Mwenyezi Mungu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji2] pole sana.
 
Yan usingeweka neno kuhusiana na kugegeda ningeshangaa sana, yan sijawah ona post yako isiyo na migegedo, we jamaa unajini mahaba mkemee haraka sana
Hahaaaaa poa mkuu nimekusoma nimekusoma
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mlitia fora mkuu
 
Masta aliwah kunifuma nilikua nimebana nyuma ya bweni sijaenda church, alfajir kigiza cha saa11. Nlivomwona akatoka nduki akaanza kunifukuza tukafika mpaka bustanini, nikampitisha kwenye majaruba ya mboga, akawa anashindwa kuruka, bahati mbaya akapita kwenye jaruba la kabeji kaikanyaga kabeji akabiringita akaangukia ndoo ya chuma iliachwa bustanini. Mie nikawah fasta nikazama church, ilipopigwa rollcall (rokoo) matata baada ya ibada hata ivo walikuta wanafunzi wote tupo kanisani. Kumbe master alipoangulia ndoo alivunjika mkono aisee
 
Elezea basi hata hueleweki lo
 
Nikiandika matukio tuliyowahi kufanya mtanijua ID yangu.

Ila dah nikikumbuka huwaga nachekaaa weeeee.. Kisha nashushia na fanta
 
Ikawaje sasa endelea kidogo
 
Kitambo sana mm nilikuwa mchoraji mzuri sasa kuna ticha akija anatuzodoa na viboko ju mpk darasa lote tukawa hamtumpendi basi mm ili kupunguza machungu akimaliza kipindi akitoka tu naenda ubaoni namchora alafu kila mwanafunzi nachukua fimbo anamchapa sasa kuna siku kasahau simu class basi anaingia ile anakuta watu tunamchapa kilichifuata sikujua nilipata fahamu afisini ya waalimu wananipepea na shati langu. Hii dunia acha tu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…