LGE2024 Kituko, Wagombea wa CCM wapiga magoti kuomba radhi kwa kutotimiza majukumu kipindi kilichopita

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yaani Kama hapo ,unapita unamtia mmoja mmoja kibao Cha shavu alafu unawaambia haya endeleeni na kampeni
 
Huyu mwenye kofia nyeusi mbona anatucheka wananchi.....
 
Sasa wanapiga magoti ya nini wakati Mchengerwa na Tamisemi yake imeshawabeba ? 🤣🤣🤣
 
Ndugu wananchi mlioombwa radhi,msiwachague hao kwa maana nyingine nyoeni vichwa vyao ngumu na wachagueni wagombea wa vyama vingine iwe fundisho kwao.Na wachape kazi kweli kweli pindi wakipewa nafasi kuwahudumia wananchi.
 
Wamshukuru sana Mchengerwa na OR TAMISEMI wanabebwa sana aisee lakini haki ingetendeka CCM wengi wangekaa benchi kujifunza nini vyama vingine vinatekeleza wajibu wake kwa Wananchi.
Sema tu sisi Watanzania ni kondoo! Tulitakiwa tulisimamie hilo la kukata watu hovyo hovyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…