Kitumbua

Kitumbua

chetuntu

R I P
Joined
Jan 10, 2011
Posts
949
Reaction score
111
Habari wadau wa lugha natatizwa na kitumbua kinachomwa, kaangwa, au pikwa? Huku uswaz tunachoma vitumbua.
 
Labda Kukaanga ama kuchoma!Ila kupika hapana!
 
Nadhani kuchoma inaendana na direct contact na moto
kupika ni kama kuchemsha na kuchanganya contents ktk stage tofauti
kukaanga inaweza kuwa ndiyo sahihi kwani inahusisha kuweka kitu katika mafuta yanayochemka
 
asante mkuu kwa maelezo mazuri, chapati je?
 
Kwa mantiki sahihi ya Inkoskaz, chapati ina-kaangwa (au fry, kwa kiinglish)!
 
Kwa mantiki sahihi ya Inkoskaz, chapati ina-kaangwa (au fry, kwa kiinglish)!

kukaanga ni kuzamisha kumafuta yaliyochemka kama chips, andazi, sambusa. Chapati haizami kumafuta.
 
Natondi yo, butu elama. Tokokutana mwanamboka !

dah uko fasi za Bujimai au shaba. Nakuona lerwaa dela foree. Unafanya lingala ya ndani kabisa mu roho. Juu vile najifunza. Im happy kupata profee hapa jf wa lingala.
 
dah uko fasi za Bujimai au shaba. Nakuona lerwaa dela foree. Unafanya lingala ya ndani kabisa mu roho. Juu vile najifunza. Im happy kupata profee hapa jf wa lingala.
kota na ndako,chetuntu
 
Hii mada imeanzia wapi na kuishia wapi? Nimeshindwa kufatilia kwa kukojua hii lugha hapa. Endeleeni lakini mtuwekee tafsiri ya kiswahili kwa faida ya wengine.

Ah! Ingawaje tumezowea kusema kuwa kitumbua huchomwa, lakini kuchoma ni pale kitu kinagusa moto moja kwa moja kama vile mahindi au mihogo; wakati kukaanga ndio neno ambalo lingepaswa kwa kitumbua.
 
Back
Top Bottom