Kitunguu swaumu; Kinga ya saratani, malaria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Kwa baadhi ya watu kitunguu saumu kina harufu mbaya, wengine huweza kuharisha, kuamsha vidonda vya tumbo au kusababisha harufu mbaya mdomoni.


KWA UFUPI




    • Kitunguu saumu ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula hapa nchini, ingawa watu wengi hukitumia kwa kuongeza harufu kwenye chakula bila kufahamu matumizi yake yenye manufaa kiafya
Harufu yake siku za sikukuu, umuhimu wake kwenye chakula kipendwacho na wengi Tanzania yaani pilau, umekifanya kuwa kiungo muhimu cha chakula nchini.

Kwa sasa umaarufu wake umeenda mbali zaidi baada ya wanasayansi kubaini kuwa kitunguu saumu kina kinga muhimu katika mwili wa binadamu, kambayo huweza kuzuia maradhi ikiwemo saratani na malaria.

Wanasayansi walibaini kuwa kitunguu saumu kina kemikali ya allicin' ambayo hutoka baada ya kukatwa au kutafunwa na husaidia kuzuia maradhi ya saratani na malaria.

Inaaminiwa kwamba kitunguu saumu huweza kupunguza athari za kemikali nyingine zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi na kuimarisha uwezo wa seli za mwili.

Utafiti umeonyesha pia kwamba huweza kusaidia kwa wale wenye matatizo ya mafua na hata kuukinga mwili dhidi ya malaria na saratani.

Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tiba cha Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic Dk Africanus Boniface anasema, kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambavyo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

"Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng'enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

"Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti," alisema Dk Boniface.

Uwezo wake kiutendaji;

"Dk Boniface anasema vitunguu swaumu vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation), kwa kubadilisha polysulfides' zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides' kwenye seli nyekundu za damu.

"Na pia husaidia udhibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine' na kupunguza madhara ya kisukari. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide' ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali," alisema.

Alisema harufu mbaya au nzuri ya kitunguu swaumu hutokana na gesi aina ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hydrogen sulfide' ambayo hutolewa baada ya kuvila.Dk Boniface anasema, kitunguu kinatibu maradhi mbalimbali kama vile: Saratani ya tumbo na utumbo mkubwa, huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation), katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu.

Athari zake mwilini

Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya ushauri nasaha, lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu yeye anasema kitunguu swaumu kina faida nyingi lakini kinaweza kuathiri mwili wa mwanadamu iwapo kikitumika wakati usiofaa.

"Ukiacha faida zake, vitunguu saumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na: Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.

Chanzo-mwananchi.co.tz




 
Asante Dokta Mzizi.Angalizo kwa wajawazito usitumie mpaka upate ushauri wa Daktari wako wa uzazi
 
kumbe kitunguu swaumu kna faida xana
Mkuu Edwin mkw Laiti ungelijuwa faida zipatikanazo kwa kula Kitunguu saumu kila siku basi usingeliacha japo kula punje moja ya Kitunguu Saumu. Kwa mfano ukitaka wewe usiumwe kila siku kula punje moja ya kitunguu saumu asubuhi kabla ya kula kitu kitakukinga hicho kitunguu saumu mpaka jioni

hutaweza kumwa na maradhi ya ajabu. soma hapa chini Baadhi ya Tiba zinazotokana kwa kutumia Kitungu Saumu mimi huwa ninakiita Kitunguu saumu kwa lugha ya kiingereza Powerful Natural Antibiotic.


Kitunguu swaumu hakikosekani katika kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa tiba.Kitunguu swaumu ni jamii ya yungiyungi.Kitunguu swaumu kilicho bora zaidi duniani ni kinachotoka misri kwasababu ya tabia ya ardhi yake na mto nail.Kitunguu swaumu kina harufu ya kipekee isiyowapendeza watu wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili hiyo maana yake kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.

Ili kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada ya kukila,kula tofaa au tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa maji yaliyotokosewa karafuu.Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani yake kukauka kabisa).


Kitunguu swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji sumu,vikojozavyo,vitoavyo safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU;

1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza

13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho

MATUMIZI NA MAANDALIZI KATIKA KUTIBU


Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu katika tiba yanategemea aina ya maradhi unayotaka kuyatibu,hivyo basi ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa tiba mbadala ili uweze kupata maelekezo sahihi ya namna ya kuandaa kulingana na ugonjwa unaokusumbua.Kumbuka kama tulivyosema awali kuwa kitunguu swaumu kikipikwa kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba unayokusudia.

Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza kuchanganywa na vitu vingine mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri n.k.kutegemea na maradhi unayotaka kuyatibu na
Ukiwa na Shida yoyote ile

Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 

Attachments

  • jinsiulivyo.jpg
    306.8 KB · Views: 412
Ahsante kwa elimu.

Asante Dokta Mzizi.Angalizo kwa wajawazito usitumie mpaka upate ushauri wa Daktari wako wa uzazi
Na huyo Mja mzito atakaye tumia dawa pasipo na kumuuliza Daktari atakuwa hana akili huyo. Wewe una mimba kisha ule dawa pasipo na kuuliza kwa Daktari utakuwa kweli unayo akili? ukiweza tembelea Blog yangu bonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Mzizimkavu tupe na tangawizi tujue faida zake.

TANGAWIZI PIA NI POWERFULL NATURAL ANTIBIOTIC


ZIJUE FAIDA YA KUTUMIA TANGAWIZI, HUTIBU MAGONJWA 72

Ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi.
Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Na kwa hapa Tanzania Tangawizi hulimwa sana mikoa ya nyanda za juu Kusini na baadhi ya mikoa kama Kilimanjaro, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara, Morogoro, na kwingineko nchini.
Pia kama bidhaa inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.
Tangawizi inatumikaje ?:
Mmea huu unaweza kuonekana kama mmea wa kawaida na watu kuutumia tu kama mazoea lakini Kiungo hiki kinaweza kutumiwa kama Dawa. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengen
ezwa unga.

Nini Faida ya Tangawizi?

Tangawizi ni mmea kati ya mimea mingi yenye maajabu, Mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.

Pia kiungo hiki kinafaida zaidi kwa Wagonjwa hasa walio athirika na Ugonjwa wa UKIMWI. Hivyo chonde kwa wale wenye matatizo kama haya wanaweza kupata faida zaidi ya Maajabu ya Mmea huu wa Tangawizi.
Jinsi ya kuitumia kama Dawa:

Tangawizi ikiwa imesagwa au Mbichi iliyopondwa pondwa inaweza kutumika kama Kinywaji kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Namna rahisi ya kuitumia Tangawizi ni katika chai, inakuwa ni mubadala wako wa majani yale meusi ya chai ambayo yenyewe huwa na kaffeina ambayo hupelekea magonjwa mengi mwilini (soma kuhusu kansa na uzito kupita kiasi kuyajuwa madhara ya kutumia majani ya chai nyeusi), Pia inaweza kutumika katika vyakula hasa nyama na mbogamboga zingine, inaweza kuongezwa katia juisi freshi pia na kuleta radha nzuri ambayo ni dawa pia.

Hutibu Magonjwa gani ?

Tangawizi husaidia yafuatayo:
Kuongeza hamu ya kula
Kupunguza kichefuchefu
Kutapika, kuharisha
Kisukari
Shinikizo la damu
Kuongeza msukumo wa damu
Kutoa sumu mwilini
Maumivu ya tumbo na
Gesi tumboni.

Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu na magonjwa mengine mengi.

Kama utakuwa makini au kuwahi kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI basi magonjwa hayo hapo juu ni kati ya Magonjwa nyemelezi yanao wasumbua sana hawa ndugu zetu hivyo wakitumia Tangawizi basi wataweza kuondokana kabisa na matatizo hayo na kuishi vizuri na kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuepukana na kulala tu kitandani.
 

Attachments

  • untitled.jpg
    27 KB · Views: 348
Na huyo Mja mzito atakaye tumia dawa pasipo na kumuuliza Daktari atakuwa hana akili huyo. Wewe una mimba kisha ule dawa pasipo na kuuliza kwa Daktari utakuwa kweli unayo akili? ukiweza tembelea Blog yangu bonyeza hapa.Mzizi Mkavu

Kaka yangu we acha tu.Huku bongo ni bora liende.Ni Mungu tu anatulinda.Mara nyingi tunatumia madawa bila ushauri wa dokta au kupimwa.Elimu ya afya wengi hawajui.Vitu vingi tunafanya kimakosa bila utaratibu na matokeo yake vinageuka sumu
 
Asante Dokta
Mzizi.Angalizo kwa wajawazito usitumie mpaka upate ushauri wa Daktari
wako wa uzazi

wazungu huwa wanasema what are you trying to insinuate? haha haaa..

ila ni vyema kukumbushana aisee!
 
Kaka yangu we acha tu.Huku bongo ni bora liende.Ni Mungu tu anatulinda.Mara nyingi tunatumia madawa bila ushauri wa dokta au kupimwa.Elimu ya afya wengi hawajui.Vitu vingi tunafanya kimakosa bila utaratibu na matokeo yake vinageuka sumu
Dawa zangu nyingi mimi ninazo zitowa ni vyakula havina Madhara kwa binadamu na wala sio sumu. Tofauti na Ma-Dawa ya Ma-Hospitali mengi ya Madawa ya Hospitalini yana sumu

yanatibu na kukuletea madhara mengine, Side effect Dawa zangu inategemea na ugonjwa wako jinsi ulivyo na ukifuata Ushauri wangu unaweza kupona na usidhurike na inabidi kabla ya kutumia ulize maswali ndio maana tumeweka hapa Hii FORUM

JAMII FORUMS. Kwa kila mtu anaye matatizo aje kuuliza Swali lake na atajibiwa ipasavyo. Sio kuona dawa nimeweka wewe ukaanza kutumia pasipo na kuuliza Maswali ukija kudhuruka shauri yako Zion Daughter
 
Kwa hiyo ukichanganya tangawizi+mdalasini+asali na kitunguu swaumu unapata nini?
 
wazungu huwa wanasema what are you trying to insinuate? haha haaa..

ila ni vyema kukumbushana aisee!

Kuna mdada yamemkuta ya kumkuta jana anaitwa kukucd .Ametoa thread hapa jukwaani.Japo kuna mambo mengine yanaweza kuchangia lakini tuwezayo kuepuka tuyaepuke.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mdada yamemkuta ya kumkuta jana anaitwa kukucd .Ametoa thread hapa jukwaani.Japo kuna mambo mengine yanaweza kuchangia lakini tuwezayo kuepuka tuyaepuke.
Mkuu Zion Daughter Mbona unaleta maneno ya mkuu.@kukucd Kwenye Thread yangu hii? bado hayaja kwisha tu? usilete umbea huku tafadhali mkuu.
 
Last edited by a moderator:

Unajua Taaluma hii ya udaktari inakuwa motivated na Upendo.Hivyo naamini kila anayetoa ushauri au dawa anatamani kuona wengine wakiwa na afya njema then wajae furaha.Ni kweli tiba mbadala nyingi hazina side effects lakini kuna special cases kama wajawazito na watoto sio kila herbs au chakula wanapaswa kula.kwa mfano tu mie niliona warning kuwa sio vizuri watoto wadogo kutumia asali japo asali ina faida nyingi kwa binadamu.
Naomba unielewe kuwa sio lengo langu kumlaumu mtu bali ningependa tusaidiane kuboresha zaidi jukwaa.Hivyo ukiona kuna walakini mahali sio lazima kupinga tushirikiane tu kuondoa tatizo.
Wito wangu kwa wote ni kuwa ukipost ushauri au dawa jaribu kutafiti na side effects ili kila mtu aelewe.
Kiroho safi kaka yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…