Zion Daughter
JF-Expert Member
- Jul 9, 2009
- 8,921
- 4,240
Mkuu Zion Daughter Mbona unaleta maneno ya mkuu.@kukucd Kwenye Thread yangu hii? bado hayaja kwisha tu? usilete umbea huku tafadhali mkuu.
Nina tatizo la kutopata choo kikubwa kikamilifu.....!!Dawa zangu nyingi mimi ninazo zitowa ni vyakula havina Madhara kwa binadamu na wala sio sumu. Tofauti na Ma-Dawa ya Ma-Hospitali mengi ya Madawa ya Hospitalini yana sumu
yanatibu na kukuletea madhara mengine, Side effect Dawa zangu inategemea na ugonjwa wako jinsi ulivyo na ukifuata Ushauri wangu unaweza kupona na usidhurike na inabidi kabla ya kutumia ulize maswali ndio maana tumeweka hapa Hii FORUM
JAMII FORUMS. Kwa kila mtu anaye matatizo aje kuuliza Swali lake na atajibiwa ipasavyo. Sio kuona dawa nimeweka wewe ukaanza kutumia pasipo na kuuliza Maswali ukija kudhuruka shauri yako Zion Daughter
Mkuu unajua kwamba hata msongo wa mawazo unasababisha ukosefu wa choo?Nina tatizo la kutopata choo kikubwa kikamilifu.....!!
Naomba msaada
Samahani kwa kuliingizia hili kwani lipo nje ya maada husika, ila nimefanya hivi ili nipate msaada kwa ukaribu zaidi
Kwa baadhi ya watu kitunguu saumu kina harufu mbaya, wengine huweza kuharisha, kuamsha vidonda vya tumbo au kusababisha harufu mbaya mdomoni.
KWA UFUPI
Harufu yake siku za sikukuu, umuhimu wake kwenye chakula kipendwacho na wengi Tanzania yaani pilau, umekifanya kuwa kiungo muhimu cha chakula nchini.
- Kitunguu saumu ni miongoni mwa viungo muhimu vya chakula hapa nchini, ingawa watu wengi hukitumia kwa kuongeza harufu kwenye chakula bila kufahamu matumizi yake yenye manufaa kiafya
Kwa sasa umaarufu wake umeenda mbali zaidi baada ya wanasayansi kubaini kuwa kitunguu saumu kina kinga muhimu katika mwili wa binadamu, kambayo huweza kuzuia maradhi ikiwemo saratani na malaria.
Wanasayansi walibaini kuwa kitunguu saumu kina kemikali ya allicin' ambayo hutoka baada ya kukatwa au kutafunwa na husaidia kuzuia maradhi ya saratani na malaria.
Inaaminiwa kwamba kitunguu saumu huweza kupunguza athari za kemikali nyingine zisizofaa mwilini hasa zitokanazo na moshi na kuimarisha uwezo wa seli za mwili.
Utafiti umeonyesha pia kwamba huweza kusaidia kwa wale wenye matatizo ya mafua na hata kuukinga mwili dhidi ya malaria na saratani.
Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tiba cha Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic Dk Africanus Boniface anasema, kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambavyo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
"Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng'enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
"Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti," alisema Dk Boniface.
Uwezo wake kiutendaji;
"Dk Boniface anasema vitunguu swaumu vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation), kwa kubadilisha polysulfides' zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides' kwenye seli nyekundu za damu.
"Na pia husaidia udhibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine' na kupunguza madhara ya kisukari. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide' ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali," alisema.
Alisema harufu mbaya au nzuri ya kitunguu swaumu hutokana na gesi aina ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hydrogen sulfide' ambayo hutolewa baada ya kuvila.Dk Boniface anasema, kitunguu kinatibu maradhi mbalimbali kama vile: Saratani ya tumbo na utumbo mkubwa, huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation), katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu.
Athari zake mwilini
Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo cha huduma ya ushauri nasaha, lishe na afya COUNSENUTH, Mary Materu yeye anasema kitunguu swaumu kina faida nyingi lakini kinaweza kuathiri mwili wa mwanadamu iwapo kikitumika wakati usiofaa.
"Ukiacha faida zake, vitunguu saumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na: Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
Chanzo-mwananchi.co.tz
Bado hilo sijafahamu mkuuMkuu unajua kwamba hata msongo wa mawazo unasababisha ukosefu wa choo?
Pole zakeHaya ya kitunguu swaumu yananikumbusha lile sakata la mdada aliyekuwa mwanachama humu akatafuna kitunguu swaumu ili apambane na chunusi usoni kwake na kuishia kuharibu mimba yake changa. Alisikitisha sana yule hasa ile kauli yake, "Nilikuwa namhitaji sana huyu kiumbe mtarajiwa azaliwe salama salmini"
Pole zake
Mwanamke mjamzito hatakiwi kula kula tu vitu hovyo