KERO Kituo Cha afya Cha WAKOREA DODOMA hakuna faragha kwa mgonjwa

KERO Kituo Cha afya Cha WAKOREA DODOMA hakuna faragha kwa mgonjwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Sela Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,992
Reaction score
8,910
Mambo vipi wakuu mbalimbali .

Nimekuja Leo baada ya salamu ni juu ya kero hii.

Katika kituo kidogo Cha matibabu kinachomilikiwa na wakorea pale Karibu na soko la majengo kumekuwa hakuna faragha kati ya mgonjwa na wagonjwa wengine ama kati ya wagonjwa na watu wengine mbalimbali wanaofika kituoni hapo.

Kwa mfano ukiwa kituoni hapo wakati unapokutana na daktari kusema matatizo Yako ya kiafya si ajabu Kuona watu walioko foleni wanakusikiliza na kukushangaa kwasababu kwanza mlango wa daktari upo wazi muda wote. Pia wakati wa kupewa madawa hali ni Ile Ile unapewa dawa kila mtu anaona. Binadamu tumeumbwa na aibu na kupenda usiri juu ya vitu kama maradhi na namna ya kusema aibu zetu kwa wataalamu.

Nb . Kituo kinatoa huduma nzuri za madawa. Mgonjwa wangu alikuwa akisumbuliwa na maradhi Fulani kwa miaka mitatu lakini baada ya kutumia dawa za kituo hicho kwa miezi sita Amepona kabisa.

Wakorea kama mpo humu hakikisheni mnabadilika la sivyo nitahakikisha naenda popote niwezapo kuhakikisha huduma zenu zinafuata sera nzuri za faragha kwa wagonjwa.
Wasalam

PXL_20251013_070031295.jpg
 
Shida ya waafrika ni majungu, uchawi, wivu, aibu na kutiana nuksi, hapo umesifia kwamba wanatoa huduma bora na hapohapo umewatia mkwara wa kuwapeleka popote wasipo kusikia matakwa yako, wenzetu wameendelea na kustaarabika wara hawaoni aibu kwa maswala muhimu ya kiafya, wewe kama unaona vipi katafute huduma sehemu tofauti acha kutilia watu kiwingu cheusi.
 
Kwahiyo boss k

Kwahiyo boss Mimi kusema ukweli kwamba faragha haizingatiwi natia kiwingu Cha ridhiki za wakorea?
 
Kama hawatazingatia hili.. nitapiga hodi kote panapohusika haiwezekani mtu wanamshangaa wanakwambia he kumbe pumbu lako Bado limevimba?
 
Kwahiyo boss k

Kwahiyo boss Mimi kusema ukweli kwamba faragha haizingatiwi natia kiwingu Cha ridhiki za wakorea?
Namana huoni, wewe kama unajari sana faragha kuliko ubora wa huduma katafute sehemu nyingine, kuwatia kiwingu ni hapo ulipowatishia kwamba utawapeleka popote, huoni kama ni mkwara mzito sana, badala yake ungewaomba kistaarabu kama ipo ndani ya uwezo wao na si vinginevyo.
 
Kwenye sekta ya Afya faragha kwa mgonjwa na mtoa huduma ni lazima.
 
Namana huoni, wewe kama unajari sana faragha kuliko ubora wa huduma katafute sehemu nyingine, kuwatia kiwingu ni hapo ulipowatishia kwamba utawapeleka popote, huoni kama ni mkwara mzito sana, badala yake ungewaomba kistaarabu kama ipo ndani ya uwezo wao na si vinginevyo.
Mkuu naheshimu mawazo Yako!
 
Nitakwenda kesho Kuona kama hali hiyo imebadilika. Kama haijabadilika nimefuatilia nimeelekezwa mamlaka husika tayari kuripoti ukiukwaji huu mkubwa wa faragha za wateja.
Nb. Kwa wale wanaohisi Nina chuki na watu hawa niwathibitishie kutoka moyoni kwamba si kweli lengo langu Mimi ni kuhakikisha usiri wa hali ya juu unazingatiwa hasa ukiwa ni kati ya mtoa huduma na mteja.
 
Back
Top Bottom