Kituo cha Afya Makuburi wahudumu wenu wa maabara wachunguzwe

Kituo cha Afya Makuburi wahudumu wenu wa maabara wachunguzwe

kangesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2023
Posts
551
Reaction score
1,063
Habari,

Niko hapa tangu asubuhi nimemsindikiza mke wangu kufungua kadi ya mama mjamzito.

Tangu nimefika muda huo, kwanza wajawazito wanaofungua kadi nao wanachanganywa na wagonjwa wa kawaida kitu ambacho ndiyo kwanza nimekiona leo hapa.

Pili nimeandikisha mapokezi tukaelekezwa maabara tukiwa na taarifa za vipimo vinavyotakiwa kuchukuliwa.

Tatizo lililopo kwa hawa wahudumu wa maabara ni kwamba wanaacha kadi za watu ambao tayari tuko hapa maabara halafu wanaenda kuchukua kadi za wagonjwa waliopo mapokezi kwaajili hiyohiyo ya vipimo. Sasa nilidhani sisi ambao tumekalishwa hapa hawatuoni, ikabidi niulize. Baada ya kuuliza wakaniambia nisiwe na haraka.

Sasa kweli mtu unakaa maabara zaidi ya saa zima na hapo bado kadi niliyoandikiwa mapokezi haijachukuliwa na siyo kwamba kuna foleni, hapana hakuna foleni hata kidogo.

Acheni hizo tabia aisee, vipimo vyenyewe gharama hazitofautiani na hospital za private.
 
Serikalini watakupotezea muda watumishi wengi hawako serious, kama unaweza nenda private tuu.
 
Back
Top Bottom