A
Anonymous
Guest
Napenda kuwasilisha malalamiko kuhusu yanayoendelea katika Kituo cha Afya Makurumla (zamani Mianzini) kilichopo Mburahati, Dar es Salaam.
Kwanza, kuna changamoto kubwa ya malipo ya overtime kwa watumishi. Tulilipwa mara ya mwisho mwezi Oktoba 2025, na tangu Novemba hadi sasa hatujalipwa kabisa, kila tunapowauliza viongozi au wahusika kuhusu malipo hayo, hupokea majibu yasiyoridhisha na wakati mwingine wanakuwa wakali badala ya kutoa ufafanuzi wa kina.
Pili, kuna tabia ya utozaji wa bili kwa baadhi ya wajawazito, hata mama anayejifungua bila kutumia huduma au vifaa vinavyostahili malipo makubwa tunaambiwa tumpe bili ya takribani Shilingi 40,000, kwa maelezo kwamba ni njia ya kuongeza mapato ya kituo.
Ni kweli kuwa kwa sasa kuna ukarabati wa majengo unaoendelea katika kituo hicho, lakini hilo halipaswi kuwa sababu ya kutotulipa watumishi stahiki za overtime ikiwa fedha hizo zimetengwa kwa matumizi hayo.
Tunaiomba Wizara ya Afya, Ofisi ya TAMISEMI pamoja na mamlaka nyingine za usimamizi kufanya uchunguzi wa kina.