SI KWELI Kituo cha kuchuja damu wagongwa wamerundikana

SI KWELI Kituo cha kuchuja damu wagongwa wamerundikana

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu nimekuwa nikikutana na sana na hii picha ikielezwa kuwa ni kutuo cha wagonjwa wanaochujwa damu. Uhalisia upoje?

1775652662291.png

HEzVuSRXMAAad2S.jpeg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram, X na Facebook kumekuwa na picha inayosambaa kuanzia mwezi Machi, 2026 na kudaiwa kuwa ni kwenye kituo cha kuchuja damu kikionesha kundi kubwa la wagonjwa wakiendelea na mchakato huo.

Mtumiaji mmoja kupitia mtandao wa Instagram aliandika kuwa;

"Hiki ni kituo cha dialysis, si spa.

Mwanzoni unaweza kudhani elimu hii ni ya kujifurahisha, mpaka pale dialysis inapokuwa suluhisho lako pekee. Tafadhali linda afya ya figo zako leo, kwa sababu hilo linaweza kuwa chaguo lako pekee baadaye."


Uhalisia wa picha hiyo

Baada ya ufuatiliaji wa kina JamiiCheck imebaini kuwa picha hiyo inaweza kuwa imetengenezwa ama kuharirirwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Unde.

Picha hiyo ina ishara zinazoashiria kuwa si picha halisi ama inaweza kuwa imetengenezwa kwa AI. Mathalani miongoni mwa ishara ama dosari zinazoonekana katika video hiyo ni;
1775655013485-png.3569445


  • Muonekano wa Nyuso na Viungo: Ukikuzia picha (zoom), baadhi ya nyuso na mikono ya watu walio nyuma zinaonekana kutokuwa na maelezo ya wazi au zina umbo lisilo la kawaida, jambo ambalo mara nyingi hutokea kwenye picha zinazotengenzwa kwa AI.
1775656496288-png.3569451

  • Vifaa vya Tiba: Mirija na nyaya zinazoonekana pembeni mwa vitanda zinaonekana kutounganishwa katika mpangilio sahihi na kutokuonekana mwisho wake katika baadhi ya maeneo. Aidha badhi ya mirirja inayoonekana kwenda kwenye baadhi ya miili ya wagonjwa inaonekana kutoingia mwilini.
1775656511488-png.3569452

  • Idadi ya Watu na Mpangilio: Mpangilio wa chumba unaonekana kuwa na msongamano mkubwa sana ambao haufuati kanuni za kawaida za usalama au nafasi katika hospitali halisi. Aidha, nyuso za wagonjwa walio nyuma zinaonekana kuwa na muundo uleule (repetitive pattern), jambo ambalo ni la kawaida kwenye picha za kuzalishwa.
1775656548549-png.3569454

  • Muundo wa Vitanda: Ingawa vitanda vinaonekana kufanana, ukiangalia kwa ukaribu magurudumu na sehemu za chini za vitanda vya mbali, utaona baadhi ya sehemu zinaonekana "kuyeyuka" au kuungana na sakafu kwa namna isiyo ya kawaida.
1775656526131-png.3569453
Back
Top Bottom