KERO Kituo cha Mabasi Nanenane - Mbeya kutokuwa na Taa zinazowaka Usiku ni kero kubwa kwa Watumiaji

KERO Kituo cha Mabasi Nanenane - Mbeya kutokuwa na Taa zinazowaka Usiku ni kero kubwa kwa Watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Kituo cha Mabasi ya Wilayani cha Nanenane kilichopo Jijini Mbeya kimegeuka kero kutokana na kukosa huduma ya taa na hivyo kuwa uasumbufu giza linapoingia.

Watumiaji wengi tumekuwa tukipata wakati mgumu kutokana na kituo hicho kukosa taa kwa muda mrefu takribani Mwaka mmoja kwa sasa.

Mamlaka husika ziko wapi mbona hamchukui hatua? Hamjui madhara yanayoweza kujitokeza kwa kukosa taa usiku?
WhatsApp Image 2025-07-08 at 19.52.28_eb80fb48.jpg

WhatsApp Image 2025-07-08 at 19.52.19_42fbfdfd.jpg

WhatsApp Image 2025-07-08 at 19.52.23_5776539f.jpg

WhatsApp Image 2025-07-08 at 19.52.27_e9b0fda7.jpg

WhatsApp Image 2025-07-08 at 19.52.18_01a4ae2f.jpg
 
Leo nimefika kituo cha mabasi Nanenane mida ya saa mbili usiku, cha kushangamza ni kwamba taa zote za stendi hazifanyi kazi na giza limetanda stendi yote kama vile sio jijini mbeya. Abiria wanakaa sehemu za kubiri abiria wameqasha tochi za simu zao. Hii haijkaa sawa kwa mamlaka zinazohusika na usinamizi wa kituo hiki. Wafanyie kazi suala hili kwa usalama wa watu wote wanaouhudumiwa hapa.
 
Ni miaka 9 tangu nipite eneo hili na hatimae Jana usiku nikapita tena pale nikielekea zangu s'wanga

Taa zote zaidi ya 31 za kutoa mwanga eneo hili nyakati za usiku hazifanyi kazi ilihali stendi inaingiza magari na kutoka muda wote na biashara zingine zinaendelea.

Wahusika muone hata aibu asee, yaani mama wa watu kapokonywa pochi tuko hapohapo bahati nzuri anadai ilikuwa na simu ndogo moja, na hii ilitokana na Giza lililotanda eneo zima la standi likitegemea taa za magari na bajaji zinazoingia humo standi.
 
Back
Top Bottom