KERO Kituo cha SGR Ruvu hakifanyi kazi kwa karibu ya mwaka sasa, ni lini TRC itakifungua?

KERO Kituo cha SGR Ruvu hakifanyi kazi kwa karibu ya mwaka sasa, ni lini TRC itakifungua?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
TRC ituambie kituo cha SGR Ruvu lini kitarejesha huduma ya kupandisha na kushusha abiria, kwa kuwa sasa ni karibu mwaka mmoja tangu kituo hicho kisimamishe huduma.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, kituo cha SGR Ruvu hakipandishi wala kushusha abiria kufuatia ajali ya treni ya mchongoko iliyotokea Oktoba 23, 2025, na kusababisha kituo hicho kusitisha huduma hadi sasa.

Hali hii imesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria waliokuwa wakikitumia kituo hicho. Wananchi tulifurahia uwekezaji wa Serikali katika kituo hicho kwa sababu ulikuwa na manufaa makubwa kwetu. Hata hivyo, kwa sasa abiria tunalazimika kutafuta usafiri mwingine ili kufika katika vituo vya Soga au Ngerengere, kutegemea safari zetu kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma. Hali hii imeongeza gharama za usafiri na usumbufu kwa wananchi.

Siku ya ajali hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, akizungumza na wanahabari katika Stesheni ya Ruvu kuhusu ajali hiyo, alisema ilitokana na changamoto za kiuendeshaji. Hata hivyo, hadi sasa TRC haijatoa taarifa ya kina kuhusu chanzo cha ajali hiyo, wala kueleza hatua zilizochukuliwa au zinazoendelea kuchukuliwa ili kutatua changamoto hiyo na kurejesha huduma katika kituo cha Ruvu.

Wananchi wa Ruvu tunaomba TRC itoe ufafanuzi kuhusu lini kituo hicho kitarejesha huduma. Pia tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati suala hili ili kusaidia kupata suluhisho, kwa kuwa hali hii imeendelea kwa muda mrefu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Ufafanuzi ~ TRC: Wananchi wawe na subira Kituo cha SGR Ruvu hakitumiki, kuna uboreshaji wa miundombinu
 
Back
Top Bottom