Mashamba Makubwa Nalima
JF-Expert Member
- Mar 19, 2024
- 4,978
- 2,411
Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Henga amesema Uchaguzi wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umefanyika kwa Haki na Uwazi, kinyume na matarajio ya wengi kutokana na mnyukano uliokuwepo mitandaoni kabla ya siku ya Uchaguzi wenyewe na iwe hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu.
"Tumefuatilia chaguzi ambazo zilizokuwa zinaendelea kwenye vyama, Chama tawala pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nakuona jinsi chaguzi zimeendeshwa, jinsi tulivyoona sisi kama waangalizi wa masuala ya demokrasia nchini. Kwanza kabisa huo utaratibu wa kuchagua ndani ya vyama unatambulika kidemokrasia na chaguzi ndani ya vyama huwa ni ishara ya Uchaguzi mkuu utakuwaje kwahiyo kama ndani kuna amani na uchaguzi mkuu mara nyingi unakuwa na amani."
"Tukianza na uchaguzi wa CHADEMA ambao ndio wa hivi karibuni zaidi, uchaguzi ule ulianza kwa heka heka nyingi za mitandaoni tukasema itakuwa hatari sana huu uchaguzi, wanagombana huyu kamtupia neno huyu ikatia wasiwasi sana watanzania kama utakuwa uchaguzi wa amani lakini kinyume na matarajio ya wengi tumeona kwamba uchaguzi umefanyika kwa amani, umefanyika kwa uwazi na hakuna aliyezulika, hakuna aliyeumia, hakuna vurugu yoyote iliyotokea. Kwenye demokrasia Haki ya kuchagua kwa usalama pia ni haki ya binadamu, ni haki ya kidemokrasia, pia tumependa ambavyo Uchaguzi umekuwa wazi aliyeshindwa ameona kabisa ameshindwa na aliyeshinda ameona kabisa ameshinda, hiyo ni zuri sana tunaweza kujifunza hata kwa uchaguzi mkuu kuwe na uwazi kwasababu demokrasia inataka uwazi"