Kituo cha television ITV Tanzania, kweli ni Super Brand

chivala

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2021
Posts
772
Reaction score
2,332
Wakuu,

Nayasema haya, siyo kwa upendeleo bali ni ukweli mtupu hata ninyi mnaweza kuwa mashuhuda jinsi ITV inavyoripoti kutoka Mahakamani kwenye kesi ya Mheshimiwa Mbowe na wenzake.

Kwenye taarifa zake za habari, ITV huweka wazi taarifa na mambo mbalimbali bila woga wala upendeleo.

Hii imefanya brand ya ITV kuendelea kuwa imara, ya kuaminika katika utoaji wa taarifa zake.
 
Ukitaka kujua kuwa super brand.
ile siku ya uchaguzi 2015,2020 live bila chenga jamaa anaonyeshwa kukimbia na box la kula.

mimi mtangazaji chizcommmmmmmmmm toka ITVvvvvvvvvvvv!
Unamaana super brand ilinywea kabisa!
 
Superbrand kwa sasa hapa bongo ni UTV tu hiyo ITV ilikua zaman bana miaka ya 2004 nikiwa mdogo ITV ilikua ikigoma nlikua nakosa raha na muda mwngne ilibidi nipande juu ya bati kurekebisha antenna kwa kujifichaficha wazee wasinione enzi hizo hapo sina hata miaka 9.

Enzi hizo nyumban kwenu kama mna TV ambayo haishiki ITV hiyo TV inakua ni sawa na radio iliyochangamka tu
 
baba wa superbrand hayupo tena.maana waandishi wa habari wanatakiwa kusifia tawala ili kupata teuzi.
unanikumbusha Mzee Abdallah Mwaipaya kasifiasifia, akalamba u DC
 
Unazingua kwa habar gan walizonazo?
 
UTV wako poa sana..Azam wanajitahidi sana..

ITV wananiachaga tu hoi na habari zao za michezo..yaani mara mashindano ya bao,kuvuta kamba..yaani
 

Thibitisha kama siyo mchagga wewe!!!!
 
UTV wako poa sana..Azam wanajitahidi sana..

ITV wananiachaga tu hoi na habari zao za michezo..yaani mara mashindano ya bao,kuvuta kamba..yaani

Hawanaga habari za michezo za maana hao ITV, hovyo kabisa, miaka yote wako ivoivo hawabadiriki. Kwenye michezo nilikuwa nafuatilia star tv kwa kipindi kile. 4now niko na smartphone cna abari nao.
 
JPM aliichukia tasnia nzima ya habari kwa sababu ya ITV.
 
Mkuu ebu achana na ilo neno enzi hizo bas uone ata aibu,
Unatuambia enz izo kama unazungumzia miaka ya 80
 
Naye lemutuz ni superbrand ,maisha yapo kasi sana
 
Kituko moyoni na research fupi tuliyo fanya na mabaharia wenzangu.
Sikweli kama ITV ni super brand mimi na mabaharia wenzangu wamesema UTV ndio superband.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…