Kituo cha Ujasiriamali na Mafunzo chazinduliwa

Kituo cha Ujasiriamali na Mafunzo chazinduliwa

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,162
Reaction score
705
Hii ilikuwa ndoto na hitaji la walio wengi - Kupata sehemu ya kufundishwa ujasiriamali, biashara na fani mbalimbali kwa muda mfupi na muda mrefu kwa gharama nafuu na muda ambao mtu yeyote anaweza.

Wilayani Temeke, Dar es salaam kimezinduliwa KITUO CHA UJASIRIAMALI NA MAFUNZO TEMEKE.

Nilichopenda hapa ni uwepo wa mafunzo ya ujasiriamali na biashara, na fani kama ususi, ujenzi, ufundi seremala, english course, computer course, ufundi umeme, ufundi vifaa vya umeme nk kwa mtu yeyote bila kujali ufaulu wa form four; yaani fursa kwa wote.

Pia ni sehemu mahususi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kupata ushauri na usaidizi katika biashara zao.

Rai yangu ni vituo kama hivi kufunguliwa vingi ili kutoa nafasi nyingi zaidi kwa wananchi wote waweze kupata mafunzo na maarifa ya kazi kisha waweze kujiajiri na kuajiriwa.

Nawapongeza Temeke kwa kuanza kuwa na kituo hiki, kitasaidia kiasi kwa Vocational Education. Naomba na wenye uwezo wa kuanza sehemu zingine waanze pia.
 
na ajira mtawapa?

Ajira zipo na kuna za kutengeneza wenyewe. Kikubwa sana hapa ni stadi, ujuzi na maarifa baada ya hapo mtu akipata uwezo anaweza kujiajiri na kuajiri wenzake.
Nimelipenda hili wazo kwa kweli
 
Back
Top Bottom