Februari 28, 2022, kituo kikuu cha wanahabari cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Walemavu ya Beijing kilianza kazi rasmi baada ya kukamilisha mabadiliko kutoka Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi.
Takriban vyombo vya habari vya uchapishaji na watangazaji 3,300 kutoka sehemu mbalimbali duniani watashiriki katika kazi ya kuripoti na kutangaza michezo hiyo.
Kituo hicho kitafunguliwa kwa vyombo vya habari kuanzia saa moja asubuhi hadi saa sita usiku kila siku.