Kituo kikuu cha Polisi Shinyanga Wamnyima ndugu yangu kanyimwa Dhamana

Kituo kikuu cha Polisi Shinyanga Wamnyima ndugu yangu kanyimwa Dhamana

monaco

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,184
Reaction score
1,778
Wakuu Amani iwe kwenu,
Mzee wangu Jana tarehe 26 September,2015.Mzee wangu amenyimwa Dhamana na Afisa aliekuwa Zamu tarehe tajwa hapo Juu!ktk Kituo cha Polisi kikuu Shinyanga,
Ana nyumba amepangisha,mpangaji alisafiri akalipia kodi nusu,Nusu,muda wa Kodi ukaisha yeye alikuwa Amesafiri,nikapata Mpangaji Mwingine kila nikimpigia hapokei simu,lengo lilikuwa kumpa habari muda umekwisha na kuna Mtu anataka kuingia ktk chumba hicho,Cha ajabu siku alikuja nikiwa sipo akahamisha vitu vyake na kuacha meza 2 tuu,na funguo akachukua,nilivyorudi nikamtafuta simu hapokei,nikaamua kubadilisha Vitasa na kuweka mezani zake 2 kibarazani,Sasa akarudi amemuweka Ndani Mzee,kisa alitaka eti kuendelea na Upangaji,na Polisi wamekataa kata kumpa Dhamani!
Msaada kwa Mwanasheria alieko Shinyanga kwa Kunyimwa Dhamana!
 
Refusha mkono hii bongo bana. tafuta mwanasheria kama unataka mzee aendelee kukaa ndani na kupoteza hela zaidi. Pole kwa yaliyokukuta
 
Refusha mkono hii bongo bana. tafuta mwanasheria kama unataka mzee aendelee kukaa ndani na kupoteza hela zaidi. Pole kwa yaliyokukuta

Ahsante Kwa Ushauri ila Mimi Nipo Dar,nimepigiwa Simu Jana hiyo hiyo jamani jinai ndo hakuna Dhamana,eti hakuna tuu Dhamana,kwanini?hawana majibu!ndo maana natafuta mwanasheria alieko Shinyanga Anisaidie kwa Hilo Mkuu!
 
Ahsante Kwa Ushauri ila Mimi Nipo Dar,nimepigiwa Simu Jana hiyo hiyo jamani jinai ndo hakuna Dhamana,eti hakuna tuu Dhamana,kwanini?hawana majibu!ndo maana natafuta mwanasheria alieko Shinyanga Anisaidie kwa Hilo Mkuu!

Hauna ndugu walioko Shinyanga wakamtoe mzee! Sina hakika ila inawezekana pia weekend inachangia polisi kutotoa dhamana. Ushauri wangu tafuta mtu aende akarefushe mkono watakubali tu hii bongolala
 
Heshima mbele..... Nilikuwa napitia magazeti nianze wiki nikakuta hii article inayohusu uboreshaji wa mikataba ya madini as commented/suggested by Mhuu wa Mkoa wa Arusha (prev in Mara).... Aisee kuna viwili hapo:
1. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kidogo upeo wa kuelea ni mdogo, au
2. Mwandishi wa habari hii ameleta part tu ya ushauri/jibu.

Hii ni sababu anaposema kuwepo na mTanzania katika kila mradi/mkataba wa madini amesahau/hajui kuna makundi matatu ya waTanzania katika miradi hii:
1. Kundi la kwanza ambalo ni kubwa ni "Wadanganyika" - Hawa ni wale wavuja jasho wa migodini ambao wanalipwa peanuts
2. Kundi la "Mafisadi" - Hawa ni wale waliotoa michongo kwa wawekezaji na kupewa 10% (or so commission/asante) kwa kuwachinja Wadanganyika
3. "Walaji kiulaini/ Watendaji" - Hawa ni wale ambao wanajaribu kuwatetea Wadanganyika lakini tatizo ni kwamba nao wana njaa so wakitaka kupioga kelele wanapewa cha juu au vijiposting serikalini/kwenye makampuni hayohayo kisha wanatulia!!!

Sasa Mhe Mkuu wa Mkoa alitakiwa awe muwazi na mkweli katika kuliongelea hili sababu kusema peke yake that '"Lazima awepo mTanzania katika kila mradi pekee" ni very VAGUE point ambayo being Mkuu wa Mkoa (miwili tayari na vijiposti vingine) inanifanya nishindwe kutambua uelewa na ufahjamu wa mzee wetu......

http://www.ippmedia.com/ipp/itv/2008/01/23/106883.html

We ulivyovunja kitasa cha mpangaji na kuweka vifaa vyake nje ulipewa dhamana na nani?
 
Maelezo yako hayaeleweki ndio maana kanyimwa dhamana

Halafu muambie akome tabia ya kutembea na mikadi ya chagadema mfukoni, ni sawa na kutembea na bangi mfukoni
 
tahadhari; wengi humu ni wapangaji ila kwa kuwa umewafata mwenyewe mameno hawatakunyima
 
Pole, dawa ya matatizo kama hayo ni kuiondoa ccm inayozalisha polisi ambao wanajifanya ni kila kitu. Hapo bila hongo ujuwe mzee wako hata kura hatapiga.
 
Nakubaliana na mchangiaji hapo juu wengi umu wapangaji sasa subiri tantalila zao hilo ni angalizo tuu,
Sikukuu na hii week end uweda imechangia kutopata dhamana kwa Mzee wako lkn ukweli utabki pale pale mna haki zote kubaki na nyumba yenu na kuchagua nani aje kupanga,Tafuta wakili atakusaidia ..
 
Pole, dawa ya matatizo kama hayo ni kuiondoa ccm inayozalisha polisi ambao wanajifanya ni kila kitu. Hapo bila hongo ujuwe mzee wako hata kura hatapiga.

We nawe lofa! kwani ccm na mapolisi ndio waliompangisha nyumba? Kwendaaa, Ndorrrrrrrooobooo! we.
 
Iila mzee wako alikosea before hajavunja kitasa olitakiwa awasiliane hata na mjmbe na shahidi yoyote kwa kuvunja kitasa anaweza kupewa hata jesi kubwa kuwa kaiba, au vitu vimepotea
 
Kuna mkuu kasema nyumba nyumba ni haki yake anaweza kuchagua wa kumpa hilo ni sawa lkn mkishamkubalia kumpangisha na yeye ana haki zake za kisheria. Until utakapoterminate au kumwandikia notice ya kuvunja mkataba, kitendo cha kuvunja kitasa na kumtolea vitu nje ni kosa la kisheria na anaweza akaambiwa kaiba mpa milioni kumi
 
Back
Top Bottom