nkawa
Senior Member
- May 11, 2009
- 181
- 10
Kampala international University, Dar es Salaam college inatarajia kuanza masomo jumatatu baada ya likizo fupi ya sikukuu ya mwaka mpya na xmas. Kuna taarifa kwamba hadi sasa Chuo hakijalipa mishahara kwa wafanyakazi wake wote wakiwemo waaliimu kwa miezi 2 sasa. Hali hii si kwa Dar es Salaam college hata University Main campus Uganda hali ni mbaya. Kuna baadhi ya waalimu walitoka nchi za Uganda na Kenya wanaoishi hapa, wako kwenye hali mbaya ya kifedha na kimaisha. Mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kuanza mwisho wa mwezi January. Nini hatima ya wanafunzi?