Kiuchumi: Faida za Kamari ni Zipi?

Kiuchumi: Faida za Kamari ni Zipi?

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
(1) Hupunguza hamasa ya uzalishaji kwa kuwafanya watu waamini kuwa wanaweza kupata pesa kwa kucheza kamari tu.

(2) Husaidia sana kuongezeka kwa idadi ya masikini na idadi ya matajir na hivyo kupanua pengo baina ya masikini na matajiri.

(3) Hutengeza maskini wengi sana kwenye jamii na kupunguza uwezo wa kufanya uvumbuzi (innovation) ndani ya jamii.

(4) Huongeza kasi ya mzunguko wa pesa kwenye jamii kutoka kwa maskini kwenda kwa matajiri
 
Wachina wanapenda kamari na pia wanapenda kufanya Kazi kwa kujituma shida ni kwetu wabongo
Sasa watu wako B+ wakitokea wajinga kama milion 20 wanapenda kamari bado wanabaki na nguvu kazi ya kutosha inayojielewa sasa hapa bongo ndo tupo less than 100m in population alafu unakuta asilimia 75 ya vijana wanapenda kamari panabaki nn sasa kwenye hii nchi ambayo unaambiwa population yetu asilimia kubwa ni vijana

Naandika hapa huku jana mkeka wangu umechanwa na team moja😂😂
 
Aliyekuambia population kubwa ni vijana amekudanganya. Population ya tanzania asilimia kubwa ni watoto 44% na ndio sababu ya umaskini . Hapo hujatoa vijana umri 18-27 ambao wengi wao wako shule au bado hawana chochote cha maana wanacho zalisha. Bado hujatoa hapo wale wanawake wanaoamini kuzaa kwa uchungu ndio kazi yao na sio shughuli za kiuchumi. Hujatoa hapo wazee. Kwa ufupi nature ya population ya tanzania ni Tegemezi na sio productive. Population ya china watoto ni wachache sana na wazalishaji ni wengi. NB hakuna nchi iliyowahi kuwa maskini kwa sababu ya betting.
 
Kiuhalisia tz tegemezi ni wengi sana,kuna watu mpaka wana familia lakin bado ni tegemezi
 
Nchi zote zilizoendelea zinaongoza kwa kamari Sasa Tanzania wacheza kamari hawana hata mitaji wanastake mia tano ndiyo waue uchumi?
 
Asante mkuu
 
(1) Hupunguza hamasa ya uzalishaji kwa kuwafanya watu waamini kuwa wanaweza kupata pesa kwa kucheza kamari tu.

(2) Husaidia sana kuongezeka kwa idadi ya masikini na idadi ya matajir na hivyo kupanua pengo baina ya masikini na matajiri.

(3) Hutengeza maskini wengi sana kwenye jamii na kupunguza uwezo wa kufanya uvumbuzi (innovation) ndani ya jamii.

(4) Huongeza kasi ya mzunguko wa pesa kwenye jamii kutoka kwa maskini kwenda kwa matajiri
(5)Huongeza idadi ya kampuni za uwekezaji wa kamari nchini hivyo kuongeza walipa kodi
...
(6)Huongeza wabia/wadhamini wa masuala ya michezo hasa timu za soka
 
NB hakuna nchi iliyowahi kuwa maskini kwa sababu ya betting.
Nchi zote zilizoendelea zinaongoza kwa kamari Sasa Tanzania wacheza kamari hawana hata mitaji wanastake mia tano ndiyo waue uchumi?
Labda analenga uchumi wa mtu binafsi.
Kama beting ni umasikini basi mataifa mengi ulaya na Amerika yangekuwa masikini maana huko ndiyo makao makuu ya kamari, mkuu Tanzania chanzo Cha umasikini ni ujinga.
Inafikirisha....
 
Kiuhalisia tz tegemezi ni wengi sana,kuna watu mpaka wana familia lakin bado ni tegemezi
Mtu ana familia na bado anatemegemea wazazi wake 😂 hiyo nchi itaendeleaje ,, afu utakuta mtu anasema serikali isikope wakati kiuhalisia wazalishaji tanzania hawafiki 20M huku wakitegemewa kulisha 65M
 
Acha maneno , njoo nikupe bure odds 1000+ za weekend ( over 1.5 goals) ukausahau umaskini wako
 
betting na yale mapombe ya yule bilionea wenu wa manayara sijui babati ni janga la kitaifa , kwa hali hii ndiomaana vijana wengi hawana tena mzuka wa kazi wanahangaika na makamari tuuuuu na kinmgine hawana hata nguvu za kiume yaani kuna kizazi kina shida sana sasahivi Mungu awasaidie tu.
 
Siku hizi radio na tv zote na Adds zote kwa simu ni juu ya Kamali na Mikopo kausha damu.
Kama Taifa tumepiga hatua kubwa kwa msaada mkubwa wa Wizara ya Mawasiliano.
 
betting na yale mapombe ya yule bilionea wenu wa manayara sijui babati ni janga la kitaifa , kwa hali hii ndiomaana vijana wengi hawana tena mzuka wa kazi wanahangaika na makamari tuuuuu na kinmgine hawana hata nguvu za kiume yaani kuna kizazi kina shida sana sasahivi Mungu awasaidie tu.
Kazi zipi mkuu
 
Back
Top Bottom