baz kaiza
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 14,971
- 18,641
Ukingalia namna Nchimbi mwenendo wa Nchimbi na CCM naweza kusema samia alimwitaji zaidi Nchimbi kuliko Nchimbi alivyokua anamuhitaji Samia. Pamoja na mapungufu ya Nchimbi lakini Samia alitakiwa kumvumilia nchimbi mpaka 2030 kivipi nchimbi alikua anamsandia Samia kujitoa kwenye kina kirefu ambacho anaendelea kuzama ndani yake. Nchimbi alianza kurudisha CCM midomoni mwa wananchi kwa mazuri kama katiba mpya kukemea kesi za ovyo vitu ambavyo wananchi wanapigia kelele kila siku vitendo vya utekaji alikua angalau anarudisha imani kwa watu na kujua kwamba CCM kuna watu wema bado wapo kutokana na kipindi tulichopitia kwenye uchaguzi October 29. Samia alitakiwa kuishi na Nchimbi kinafiki hata kama hampendi au hapendi falsafa zake lakini falsafa za Nchimbi zilikua zinaendelea kuleta uhai kwenye chama na faida kwa Samia mpaka kufika 2030 naweza kusema alikua amepata kivuli kizuri cha kula upepo mpaka 2030 naweza kusema kivuli kizuri alikua Nchimbi. Ukimya wa rafiki yako unauma sana kuliko kelele za adui yako wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha bora mara mia Samia angeweza kuvumilia kelele za Nchimbi akiwa makamu wake mpaka mda wake ungeisha vizuri. CCM imejaa wanafiki vibaya mno bora mara mia Nchimbi alijimbanua kutoka kwenye unafiki wa wana CCM walio wengi ndani ya chama. Sasa wanasema ujanja mwingi mbele Giza sasa hivi Samia atakua anaishi bila kujua adui yake ni yupi na rafiki wa kweli ni yupi . Huwezi kubadilisha DG wa Tiss wa nne ndani ya miaka yako mitano ukasema kuna usalama hapo uongo. Kuna kisa cha mvuta bangi mmoja walimwambia kichwa chako bagi hakiwezi sasa kuna siku amevuta zake bangi kwenye ghetto lake ukafika mda akataka kutoka kwenda kutembea sasa akasema nikitembea na ufunguo naweza kuupoteza akafunga kitasa wakati anatoka akasuma dirisha akapitisha mkono akarusha funguo ndani na dirisha lina vyuma akajikuta amejifungia nje ya nyumba yake. Ujanja mwingi mbele giza.