PreGE2025 Kiujumla wanaojitoa sasa Chadema ni wasaka madaraka, usishangae baada ya uchaguzi kwisha wakataka kurejea tena Chadema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,120
Njaa hainaga simile ukishaiendekeza. Lile kundi la G55 baada ya kugundua hakuna namna mpango wa 'nusu mkate' (kupewa bakishishi ya madaraka kupitia Chadema kwa fadhila za CCM) kuweza kutekelezwa chini ya uongozi wa Lissu, wakaona isiwe tabu maana msimu wa 'mvua' umefika, hivyo wakichelewa tu hawatavuna chochote, wakaamua kutangaza kujitoa.

Ukiwaangalia kwa machoni na kuwasikiliza kwa umakini mkubwa sana, utagundua haya mambo matatu:
1. Wamekaririshwa cha kusema na kufanya (staged).
2. Hawajui kwa hakika nini hatma yao kisiasa (Wanasikilizia).
3. Wamehaidiwa kitu kizuri bila kuhakikishiwa kupewa hicho kitu (Wamekaa kimtego mnoo).

Kwa kuwa CCM ni ile ile (genge la wahuni wa kisiasa lililoshikiria madaraka), siasa ni mchezo wa kudumu kimaisha kwa mwanasiasa na madaraka ni mvinyo mtamu wenye ulevi endelevu (addiction), kuna uwezekano mkubwa sana, watu hao hao, wengi wao wakataka tena kurejea Chadema ili wafanye siasa baada ya uchaguzi kwisha (na wao kuambulia sifuri) ama ikiwa mazingira ya kisiasa kubadilika.

Mfano mzuri ni uchaguzi wa 2015 ambapo kulikuwa kuna kundi kubwa la wanaCCM lililojitangaza kuondoka CCM na kuhamia upinzani, baada ya uchaguzi kwisha taratibu lilianza upya kurejea CCM. Hapa nazingumzia watu kama Edward Lowassa, Fredrick Sumaye etc.

Upande wa pili walikuwepo pia wapinzani walioamua kujiondoa kwenye upinzani 2015 ili kuipa nguvu CCM, lakini baadaye likarejea tena upinzani. Hapa nazungumzia mtu kama Profesa Lipumba, Dr. Wilbroad Slaa.
 
Wapuuzi walikuwa wanatumia chadema kama ngazi ya ubunge. Angalia hao watu wote target yao ilikuwa ubunge, ndio maana NRNE kwao inakuwa ngumu kwa sababu inazuia objective ya kutumikia matumbo yao
 
June Chadema wanarejeshwa kwenye Uchaguzi John Mrema atakuwa wa kwanza kurejea
 
Kwani wanaobaki hawataki madaraka?.Au unadhani hizi kelele za No reform no election lengo ni nini au unadhani nikwaajili yakucheza mdundiko.Wanaobaki wanatakiwa kupambana chama kiungwe mkono sio kushambulia wanaotoka kwasababu haziwasaidii chochote kwasababu siasa ni mchezo wa fursa kwa wote na kila mtu kwenye siasa ana maisha na maamuzi yake.Wakati chadema inaanzishwa ilichukua wanachama wa vyama vingine vilivyokuwepo iweje hawa wanapojitoa muwaone wakosaji wakati ndivyo siasa zilivyo.ujinga wa kuwashambulia hautawasaidia kitu zaidi ya nyie wenyewe kuonekana mna akili za kitoto kwakugeuza siasa uadui na chuki wakati hapo mwanzo mlikua pamoja na kuna siku tena mtakua pamoja.
 
Njaa hainaga simile ukishaiendekeza. Lile kundi la G55 baada ya kugundua hakuna namna mpango wa 'nusu mkate' (kupewa bakishishi ya madaraka kupitia Chadema kwa fadhila za CCM) kuweza kutekelezwa chini ya uongozi wa Lissu, wakaona isiwe tabu maana msimu wa 'mvua' umefika, hivyo wakichelewa tu hawatavuna chochote, wakaamua kutangaza kujitoa.

Ukiwaangalia kwa machoni na kuwasikiliza kwa umakini mkubwa sana, utagundua haya mambo matatu:
1. Wamekaririshwa cha kusema na kufanya (staged).
2. Hawajui kwa hakika nini hatma yao kisiasa (Wanasikilizia).
3. Wamehaidiwa kitu kizuri bila kuhakikishiwa kupewa hicho kitu (Wamekaa kimtego mnoo).

Kwa kuwa CCM ni ile ile (genge la wahuni wa kisiasa lililoshikiria madaraka), siasa ni mchezo wa kudumu kimaisha kwa mwanasiasa na madaraka ni mvinyo mtamu wenye ulevi endelevu (addiction), kuna uwezekano mkubwa sana, watu hao hao, wengi wao wakataka tena kurejea Chadema ili wafanye siasa baada ya uchaguzi kwisha (na wao kuambulia sifuri) ama ikiwa mazingira ya kisiasa kubadilika.

Mfano mzuri ni uchaguzi wa 2015 ambapo kulikuwa kuna kundi kubwa la wanaCCM lililojitangaza kuondoka CCM na kuhamia upinzani, baada ya uchaguzi kwisha taratibu lilianza upya kurejea CCM. Hapa nazingumzia watu kama Edward Lowassa, Fredrick Sumaye etc.

Upande wa pili walikuwepo pia wapinzani walioamua kujiondoa kwenye upinzani 2015 ili kuipa nguvu CCM, lakini baadaye likarejea tena upinzani. Hapa nazungumzia mtu kama Profesa Lipumba, Dr. Wilbroad Slaa.
Ni kipindi cha kusalitiana.CCM nao wataanza hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom