Kiukweli asilimia ya mshahara kupanda haikutakiwa kutangazwa ili kudhibiti mfumuko wa bei

Wanapenda kusifiwa sana kumbe wanaharibu.

Hali ya kiuchumi ni mbaya bado watu wanatangaza ongezeko la asilimia kubwa namna hii??

Mnataka kuangamiza watu nyie.
Hali ya uchumi ni mbaya kwako

tutoleeni upumbavu wenu
 

Toa mfano wa mwaka ambao JK hakutangaza nyongeza ya mshahara? Acha kupotosha.

Bei ya vitu inapanda kutokana na supply and demand full stop.. Hayo yako hayapo kwenye kanuni za uchumi.
 
Afu si nyingi ata inayongezeka ni 23% ya kima cha chini. Ambayo ata dar kigoma haitoshi nauli
 
Jiulize maswali yafuatayo kwanza
Ukiongeza mshahara bila kutangaza wafanyabiashara hawatajua?
Watumishi wa serikali jumla wako wangapi?
Tangu mwaka jana bidhaa zinazidi kupanda bei, kulikuwa na ongezeko la mishahara?
 
Ila hii nchi 👐 hakuna jema kabisa
 
Sure HAPA WANYONGE NDO TUTAUMIA
Hakuna mfanyabiashara atakayepandisha bei kisa kasikia wafanyakazi wameongezwa mshahara. Bei zinapanda automatically kulingana uhitaji na upatikanaji.

Wafanyakazi serikalini ni wachache sana ukilinganisha na population kwa ujumla (~60milioni)
 
kabla hata ya kutangazwa kwa ongezeko jipya la mshahara jeh! hakukua na mfumko wa bei?

gharama za maisha zimepanda kabla hata ya kuingezeka kwa mshahara sasa sijui ndugu umeandika makitu gani?

halafu kimsingi kila mtu na falsafa zake mzee wa msogo alikuwa hatangazi lakini kwani watu walikuwa hawajui kama mshahara umepanda?
 
Hakuna mfanyabiashara atakayepandisha bei kisa kasikia wafanyakazi wameongezwa mshahara. Bei zinapanda automatically kulingana uhitaji na upatikanaji.

Wafanyakazi serikalini ni wachache sana ukilinganisha na population kwa ujumla (~60milioni)
Unajua serikali inatumia sh ngap kulipa mishahara watumishi.. ? Kwa mujibu wa bajeti Mpya mishahara inachukua tirion 9.8 HIV, na bajeti ya serikal ni tirion 40. Ni asilimia ngap Ambyo wafanyakaz wanapta na effect Yao kwenye uchumi.???
Na ukumbuke huduma zotë zinaweza kutotolewa ila bajeti ya mishahara iko palë palë. Rud Shule mdogo wangu. Don't underestimate contribution of public servant in economy
 
Ni bidhaa gani ambazo hutaki zipande bei? Mchele, unga, maharage na mihogo? Hujui kwamba wakulima wananunua pembejeo kwa bei ghali? Hujui kwamba huu mwaka mvua hazikua nzuri kwa hiyo tumewekeza vingi lakini mavuno ni haba?!
Kanuni za uchumi ni kupandisha kila idara na kila sekta, otherwise hata kama nyie wafanyakazi wa uma ndo peke yenu wenye pesa, bado uchumi utakwama kwingine, na taifa litakwama tu! Na kama hujui wale wazalishaji wa bidhaa, ambazo hutaki zipande sambamba na mshahara wako, hao hao ni shangazi zako na wajomba zako! Kama ukiwa na pesa na wao hawana, watakuomba, watakukopa au wakuibie, na ikishindikana wakuroge, mkose wote!
 
Havina uhusiano, bei upanda kulingana na nguvu ya soko. Mbona mafuta ya kula, nauli, vitu dukani vimepanda kabla ya mshahara
 
Huku kupanda kwa vitu yale maduka ya Majeshi yange rudishwa.
 
Damned if you do, damned if you don't.

Aliposema "lile jambo letu lipo" akasemwa
Leo kasema ongezeko ni kiasi gani anasemwa
 
Kila tatizo ni fursa, tunapaswa tuzitumie fursa zinazotokana na "mfumuko wa bei" kuzifanya mafanikio.

"Necessity is the mother of invention" Uhitaji (umuhimu) ni mama wa uvumbuzi.

Kupanda (mfumuko wa bei) kwa bei za bidhaa inatubidi wadau wa ujenzi tubuni mbinu mpya za kupunguza gharama za ujenzi bila kuathiri ubora (quality and standards). Hapa darasa la ujenzi la waja wema, tumebuni aina ya ujenzi wa ngazi za kipekee, zenye kukidi viwango na kupitiliza viwango na zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu. Bofya link ujionee: Darasa la ujenzi la Madrassatul Abraar latunukiwa Tuzo ya ubunifu wa ujenzi kutoka Shirika la Uingereza.
 
Hakuna uhusiano bei ya vitu utegemea upatikanaji, kodi, uhitaji.
Mshahara hauna uhusiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…