Kiukweli Marais wastaafu wa Tanzania ni wanyonge wenzetu, utajiri aliouacha Moi Kenya unadhihirisha ubepari wa nchi hiyo!

Kiukweli Marais wastaafu wa Tanzania ni wanyonge wenzetu, utajiri aliouacha Moi Kenya unadhihirisha ubepari wa nchi hiyo!

Umenena ukweli kabisa
Ukimwondoa Mwl. Nyerere pengine na Mh. Mwinyi. Wengine ni matajiri wa kutupwa ila hawana uthubutu wa kuonyesha mali na fedha walizojilimbikizia kwa njia za ufisadi mkubwa sehemu mbalimbali ulimwenguni. Ukiona Trump anaziita nchi za Afrika kama "shithole" kupitia viongozi wake, basi tambua kuwa wanajifanya kuwa ni wenye maisha ya kawaida kumbe nyuma ya pazia ni kinyume chake kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Hujui lolote kuhusu ukwasi walionao hao wastaafu wako! Laiti ingekuwa accounts zao huko uswiss, America na ulaya Zina salio la kiasi gani usingeandika mashudu yako hayo!
Magu aliwahi toa Rai kuwa wenye mapesa yao nje wayalete nchini ili kuuboost uchumi na kusaidia kutoa ajira! Sina uhakika Kama ulimwelewa na au alikuwa anawaambia kina nani! Kama hata joka la makengeza Lina mabilioni huko nje je, wao wanashindwa Nini. Kina Jamal walikataa kurudi kuzikwa nchini na alizikwa Canada Kama raia wa Canada ilihali alikuwa waziri wa fedha wa Tanzania! Unaijua sababu? Waliwekeza mapesa mengi huko waliyoyakwapua na familia yake inaishi huko ikila nchi!
Mzee Jamal gani aliwekeza mapesa Canada kiasi cha kukataa kuja kuzikwa Tanzania?
Huyo Mzee jamal alikufa maskini kabisa kiasi cha kushindwa kumudu gharama za matibabu yake hadi kuombewa msaada na Nyerere kwa serikali ya Canada.

Acheni habari za kizushi. Soma hapo kwenye hii thread ipo humu humu JF iliyoelezea jinsi alivyokufa maskini.
Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake
KUUMWA KWA MZEE JAMAL,AGIZO LA MWL NYERERE NA UTEKELEZAJI WA MEMBE KUHUSU SERA YA URAIA PACHA.

Jana niliahidi kuendelea na simulizi kuhusu mambo kadhaa yamhuhusuyo Ndg.Bernard Kamilius Membe na siasa za nchi yetu.Simulizi hizi zipo katika mtindo wa "series".Kila "episode" ya "series" hizi itahusisha matukio muhimu yasiyo maarufu kwa watu wengi lakini yana mvuto wa kipekee katika wasifu wa Ndg.Bernard Kamilius Membe.

Nitaendelea nilipoishia jana......

Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kumpatia majibu Ndg.Bernard Kamilius Membe kuhusu swali la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya ushiriki wa vijana kwenye kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 uliojumuisha vyama vingi,likaibuka suala la ugonjwa na matibabu ya aliyewahi kuwa waziri wake wa fedha enzi za uongozi wake aliyeitwa Mzee Jamal.

Kwa vijana wa sasa wasiomjua Mzee Jamal huyu alikuwa waziri wa fedha katika serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.Alikuwa na asili ya kihindi.Lakini ni mzawa wa nchini Tanzania.

Alikuwa mfanyabiashara,raia mwema aliyeshiriki katika mapambano ya kupigania uhuru tangu enzi za TANU hadi pale ilipozaliwa CCM.

Baadaye aliachana na siasa.Akarejea katika shughuli zake binafsi.Na hata umri ulipomtupa mkono alisafiri kuishi na mwanaye nchini Canada hadi umauti ulipomfika.Alikuwa rafiki mkubwa wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Wakati wa mazungumzo yao mengine Ndg.Bernard Kamilius Membe alimjulisha Mwl.Julius Kambarage Nyerere juu ya hali ya afya ya rafiki yake wa muda mrefu Mzee Jamal.

Kwa wakati huo Mzee Jamal alikuwa akiumwa sana.Na gharama za matibabu zilikuwa juu sana nchini Canada hivyo kufanya familia yake kushindwa kuzimudu ipasavyo.

Pamoja na kuwa mfanyabiashara miaka ya nyuma na kuwahi kuwa waziri wa fedha enzi za Mwl.Julius Kambarage Nyerere lakini hakuweza kujilimbikizia mali wala kukwepa kodi.

Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuelezwa na Ndg.Bernard Kamilius Membe kuhusu kuumwa kwa Mzee Jamal ilibidi Mwl.Julius Kambarage Nyerere aombe ofisi za ubalozi kupelekwa siku inayofuata kumwona na kumjulia hali rafiki yake Mzee Jamal.

Siku iliyofuatia alipelekwa akiambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe.Hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal haikuwa nzuri sana.Mtoto wake alilia sana akiomba msaada wa kugharamiwa matibabu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ubalozi uliopo Canada.

Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliumizwa sana na hali ile.Akamwagiza Ndg.Bernard Kamilius Membe kuzungumza na Balozi wetu wakati huo nchini Canada ili apate mihadi ya kuonana na waziri mkuu wa Canada wa wakati huo ambaye alikuwa na mahusiano naye mazuri.Nia ni kuzungumzia suala la matibabu ya Mzee Jamal.

Baada ya waziri mkuu wa Canada kuridhia kuonana na Mwl.Julius Kambarage Nyerere siku ilipowadia Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe katika kikao kila na waziri mkuu wa Canada.

Mazungumzo yalikuwa na ajenda moja tu ya matibabu ya Mzee Jamal.Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliomba msaada wa matibabu bure kwa Mzee Jamal kwasababu familia yake haimudu gharama zake na hali ya Mzee Jamal inazidi kuwa mbaya kila siku iendayo kwa Mungu.

Waziri mkuu wa Canada aliridhia kusaidia gharama za matibabu ya Mzee Jamal lakini akishauri kuwa kwakuwa nchini kwake matibabu ni bure(kwa wakati ule-sijajua kwasasa)lakini kwa mtu mwenye uraia hivyobasi akaagiza Mzee Jamal apatiwe hati ya kusafiria ya Canada na uraia kamili wa Canada.Alifanya hivi kwasababu wao wanaridhia uraia pacha(dual citizenship)lakini kwakuwa Tanzania hatuna sera hii basi ni lazima Mzee Jamal aukane uraia wake wa Tanzania na kupatiwa wa Canada.

Kwa mazingira ya wakati ule Mwl.Julius Kambarage Nyerere na familia ya Mzee Jamal hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kukubaliana na ushauri wa waziri mkuu wa Canada ili kuokoa maisha ya Mzee Jamal.

Baada ya kikao kile jukumu la kushughulikia suala la uraia wa Mzee Jamal likakabidhiwa kwa mamlaka husika ya serikali ya Canada na ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pale Canada ukawa na jukumu la kuwasilisha nyaraka muhimu za Mzee Jamal zitakazosaidia kuthibitisha uraia wake wa Tanzania kabla ya kuhamia katika uraia wa Canada.Na ubalozi ukampatia jukumu la kuratibu hili suala Ndg.Bernard Kamilius Membe.

Kwakuwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere alikuwa na majukumu mengine katika hizo ziara zake ilimlazimu aendelee na majukumu hayo.Lakini aliambatana na Ndg.Bernard Kamilius Membe kwenda kumuaga Mzee Jamal na familia yake.Wakati akiwa uwanja wa ndege wa nchini Canada baada ya kutoka kumuaga Mzee Jamal na familia yake akielekea nchini Marekani Mwl.Julius Kambarage Nyerere alimwambia Ndg.Bernard Kamilius Membe kuwa ipo haja ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia suala la uraia pacha(dual citizenship)ambao wakati wa uongozi wake waliukataa lakini changamoto ya suala la matibabu ya Mzee Jamal limempa tafakuri kubwa sana.

Siku chache mbeleni tangu Mwl.Julius Kambarage Nyerere aondoke kuelekea nchini Marekani huku nyuma Ndg.Bernard Kamilius Membe kwa kushirikiana na serikali ya nchini Canada na ofisi za ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada walifanikisha kupatikana kwa uraia kamili wa Canada wa Mzee Jamal na kuijulisha familia ya Mzee Jamal kuwa wamwandae baba yao kwa ajili ya kufuatwa akaanze matibabu chini ya uangalizi wa serikali ya Canada kwa maelekezo ya waziri mkuu wa Canada.

Siku ya kwenda kumchukua Mzee Jamal ili akaanze matibabu Ndg.Bernard Kamilius Membe akiambatana na ujumbe wa serikali ya Canada nyumbani kwa Mzee Jamal kwa bahati mbaya walipofika tu wakakuta msiba.Mzee Jamal alikuwa kafariki muda mchache kabla ya wao kufika pale.Lilikuwa ni pigo kubwa kwa familia,serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Canada.Kubwa zaidi Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliumia sana alipopata zile taarifa.Rafiki yake mkubwa alikuwa kaaga dunia.

Na hii ndio ikawa sababu kuu ya Ndg.Bernard Kamilius Membe kuwasilisha hoja kuwa katika mchakato wa katiba mpya wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kiwepo kipengele kinachozungumzia suala la uraia pacha(dual citizenship).

Na alitoa sababu muhimu zenye mashiko ili uraia pacha(dual citizenship)iwe ni haki ya kila mtanzania huku suala la Mzee Jamal ikiwa ni moja kati ya "precedents" zinayoishi hadi leo.

Nihitimishe kwa kusema tu kwamba uraia pacha(dual citizenship)haikuwa hoja binafsi ya Ndg.Bernard Kamilius Membe bali ilikuwa na chimbuko lake.Na uzuri wa hoja hii Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliweza kumshirikisha hata Mzee Kingunge Ngombale Mwiru miaka ile wakati akimwelezea hali aliyomkuta nayo Mzee Jamal nchini Canada kabla ya umauti kumfika.

Je unajua kwamba "wanamtandao" walikuwa watano tu?

Tukutane tena kesho muda kama huu.......
 
Back
Top Bottom