Kiukweli, Simba wameshazoea kuliabisha taifa huko ugenini. Tumechoka!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Katika miaka ya karibuni, Simba SC imekuwa ni klabu ambayo ilikuwa ikiwakilisha taifa letu kwenye michuano ya kimataifa-ngazi ya klabu bingwa Afrika. Pamoja na kuwa rekodi nzuri katika uwanja wa Mkapa hapa Dar inapowakaribisha wapinzani wao wageni, Simba imekuwa ikiliaibisha taifa hili kwa vipigo vya paka mwizi huko ugenini.

Kwa kumbukumbu za miaka ya karibuni Simba walichezea kichapo cha 5-0 na Al Ahly ya Misri; 5-0 na AS Vita Club ya DRC; 4-1 na TP Mazembe ya DRC na 4-0 na Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini. Simba wafahamu kuwa wanapocheza ugenini wanabeba taswira na heshima ya nchi yetu. Kupigwa mabao mengi ni kuliaibisha taifa.

Hata kama Simba inapata ushindi kwa Mkapa, iache mara moja kutuaibisha ugenini. Tumechoka!
 
Solution ni wao pia kufunga mabao mengi wakiwa nyumbani. Kwani hawana uwezo huo?

Ukifungwa mabao mengi ugenini, nawe pia funga mabao mengi nyumbani. Problem solved!
 
Huwajui manunu ww ngoja waamke mana toka juzi hawatoki kitandani
 
Wakati Simba inaliaibisha taifa, timu nyingine zinafanya kitu gani cha maana?! Utopolo pro max!
 
Kwani Simba ni Taifa stars mkuu?? Mbon kama unaumia sana simba kufungwa,kama vp peleka timu yako ambayo haitakuaibisha kweny nchi za ugenin..
 
Waliwahi pia kupigwa 4 - 0 na Recreativo do Libolo ya Angola mwaka 2013
 

Simba anakwenda kuishangaza dunia - lazima ale 5 dadadeq - kipindi cha kwanza 3 na pili 2 akasimulie kwao.
 
Kuna uongo wowote hapo?
Ndio mleta mada ni muongongo na hajui.
Kwenye soka kufungwa kwa klabu ya soka sio kuliabisha taifa bali ni sehemu ya mchezo,hata timu za taifa za nchi zinafungwa sembuse klabu!
Kama hujui soka hujui tu.
Simba tutapindua meza,ni ngumu kupindua lakini kwa klabu ya Simba ni rahisi.
Simba nguvu moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…