Kiungo amvamia kocha na kumshindilia mangumi

Kiungo amvamia kocha na kumshindilia mangumi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
kiungo1.jpg

kiungo2.jpg

Kiungo wa timu ya daraja la kwanza nchini Scotland ya Inverness, Liam Polworth ametoa kali ya mwaka baada ya kumshindilia kocha wake ngumi wakati wakiwa katika mechi.
Kocha Scott Kellacher alilazimika kujilinda kwa kila namna wakati Polworth akimshambulia akiwa katika benchi. Kabla ya kumshambulia kocha wake, Polworth alifunga bao la pili na mechi iliisha wakishinda kwa mabao 3-1.

Hasira za Polworth ,22, ziliibuka baada ya kocha wake kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine wakati timu yao ilipishinda dhidi ya Highlanders katika michuano ya Kombe la Irn-Bru hatua ya robo fainali.

Polworth alitoka moja kwa moja hadi katika benchi na kuanza kumlaumu kocha wake kuwa pamoja na kufunga bao, bado alimtoa nje.

Kocha wake alipojaribu kumuelewesha, alianza kumshambulia kwa ngumi za kutosha hadi waliokuwa katika benchi kuingilia na kuamua ugomvi huo.

Chanzo: Saleh Jembe
 
Duh!! Hiyo ni zaidi ya ligi yetu uku bongo ya daraja la kwanza.
 
Ha ha ha hataki ujinga ujinga safi.ingawa mmh nidhamu hana itamtesa hyo
 
Hahah sipati picha ingekuwa Africa. Wangetunanga sana hawa jamaa.
 
Alimpa ndochi kadhaa
[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji122] [emoji122] [emoji122] Mkuu una umri gani....umelikumbuka hilo neno "NDOCHI"...

We kitambo hapa JIJINI...!!
 
Hahah sipati picha ingekuwa Africa. Wangetunanga sana hawa jamaa.
Sio Afrika tu,angekuwa mchezaji mwenye asili ya Africa, wangeandika sana. Rejea ya Mario Baloteli 'superMario,
 
Dahh naona jamaa akifungiwa kwa muda...thn baadae atang'aaa sanaaa...
Kiki atapata na itamsaidia piaa
 
Back
Top Bottom