Kiungo mtukutu, Gennaro Gattuso kuwa kocha wa AC Milan baada ya kufukuzwa kwa kocha aliyekuwepo

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971


Timu ya AC Milan imemtimua kocha Vincenzo Montella na badala yake imempa usukani kukisimamia kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Klabu hiyo ipo katika nafasi ya 7 kwenye orodha kwenye ligi ya Serie A ikiwa na pointi 20, 18 nyuma ya mabingwa Napoli, baada ya ushindani wa ushindi mara mbili pekee wa ligi katika michuano yao ya nyuma.

Walitoka sare ya 0-0 na Torino nyumbani siku ya Jumapili na wameshindwa mechi zao 6 kati ya 14 msimu huu.

Gattuso, ambaye alikuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan anapokea wadhifa huo kutoka kuwa msimamizi wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 19 wa klabu hiyo.

AC Milan, ambao wameshinda taji hilo la Italia mara 18 na ni mabingwa mara 7 wa Ulaya, hawajawahi kuibuka katika nafasi tatu za juu katika ligi ya Serie A tangu 2013.

Wametumia pauni milioni 205 kuwasajili wachezaji wapya tangu mfanyabiashara wa kichina Li Yonghong kuidhibiti klabu hiyo Aprili mwaka jana.
 
Safi kabisa. Japo nipo upande wa Juve na inter ya Mauro Lcardi
 
Huyu anaweza kuwapiga ngumi wachezaji wake aisee,

Kila la kheri kwake
Ukivuta picha ya akina giovin trapattoni, cesare maldin,fabio capello na arrigo sacchi mpaka enzi za kuwatumia wachezaji wao miaka ya karibuni kama seedorf na pippo inzaghi na hatimae leo genarro gatusso hii timu imepitia tamu na chungu kama ilivyo kawaida ya soka ila kiukweli siioni juhudi ya kuirudisha AC milan ya ukweli ingawa muda ni mwalimu mkuu ila sijashawishika kuiona timu japo inatoa upinzani wa maana.
 
AC Milan ya sasa imekuwa laini mno aisee,

Wasije kuwatumia wachezaji wao wawe makocha. Naona majirani zao Inter Milan msimu wako vizuri

Ngoja tuone Gattuso atafanya nini
 
hii timu imenunuliwa na wachina na ilianza ligi vizuri tu sijui hata balaa gani limeikumba aiseeeee mpaka kuwa na matokeo mabovu
 
Genaro gattuso one of the taff/fantastic midfielders in his career!
Hapo hawezi leta jipya ndani ac Milan, kocha aliyekuwepo he is very professional but team inapata matokeo mabovu pamoja na usajili wa mabilioni walioufanya.
Wana safari ndefu
# team Lorenzo insigne
 
Yatakuwa yale yale ya Seedorf,ni heri timu wampe Ancelot kwa mara nyingine.
 
Yatakuwa yale yale ya Seedorf,ni heri timu wampe Ancelot kwa mara nyingine.
ila seedorf alikuwa ni kocha mzuri sana kwa ac milan, unaiona kabisa ac milan ikicheza soka safi na la kivutia na aliisogeza timu hadi nafasi ya saba kwa muda mfupi tu aliyofundisha milan. Wangempa muda angeifikisha mbali ac milan lakini berllusconi na mwenzie gallian wakakosa uvumilivu wakamtimua. Kufukuzwa kwa montella ni sahihi sana maana timu haipati matokeo mazuri na lengo lao msimu huu kuingia top 4, lakini kumpa kazi Gattuso ni kamari nyingine kubwa zaidi hata kama kafundisha ac milan primavera. bora wangepata kocha mwenye uzoefu
 
Inzaghi, Seedorf na sasa Gattuso wote wataangukia pua katika career ya ukocha. Tatizo wanakuja kwa pupa na kwa haraka, Zizu au Guardiola hawakuanza ghafla tu ukocha walijifunza, walipitia apprenticeship under makocha wengine nguli, walifundisha timu B za vilabu vyao kupata experience kabla ya kuwa makocha wa timu A. Hawa wengine wataangukia pua that's a given
 
Mfano mzuri ni Allan Sheare aliyefanya maamuzi mabovu kukubali kuifundisha new castle iliyokuwa ina hali mbaya akaishia kuishusha daraja.

Conte tu ndio cocha wa kitaliano aliyebakia baada ya kizazi cha kina lippi na capello kupita
 
AC Milan ya sasa imekuwa laini mno aisee,

Wasije kuwatumia wachezaji wao wawe makocha. Naona majirani zao Inter Milan msimu wako vizuri

Ngoja tuone Gattuso atafanya nini
Kama hakuna uwekezaji wa maana hawezi kufanya lolote Berlusconi alikuwa mthubutu na mwendawazimu wa mafanikio mpaka akaweza kuifanya rosonelli ikawa moto kwa vipindi tofauti manguli kama akina frank rijkarď na nduguze Basten na guilt mpaka kina the phenomeno achilia mbali George mannah osmanu oppong weah palikuwa pazuri sana rossoneri sasa huu uwekezaji usiwe wa ujanja ujanja hapo genarro utamtaka na ile amsha amsha yake
 
Hao jamaa toka China wamewekazana Sana msimu huu, Ila naona wachezaji bado hawatoi kile wawekezaji wanachotaka.

Tuone mabadiliko kutoka Kwa Gattuso sasa.
 
Hao jamaa toka China wamewekazana Sana msimu huu, Ila naona wachezaji bado hawatoi kile wawekezaji wanachotaka.

Tuone mabadiliko kutoka Kwa Gattuso sasa.
Uwekezaji mkubwa Unahusisha pia ushawishi wa wachezaji kuja hapo San siro hilo ni jambo jema sana sasa ushawishi sio wa pesa tu hata namna club imepanga nini ndani ya muda gani ili wavutike watu kuja hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…