Kiungo wa Simba Sc Fabrice Ngoma,ataondoka msimu huu kwenda Moja ya timu nchini Morroco

Kiungo wa Simba Sc Fabrice Ngoma,ataondoka msimu huu kwenda Moja ya timu nchini Morroco

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kiungo wa Simba Fabrice Ngoma hatakuwa msimbazi msimu ujao, Ngoma anaondoka Simba akiwa hajatwaa Taji kubwa kama ligi kuu au FA.

Taarifa zisizo rasmi zinasema Fabrice Ngoma atajiunga na Moja ya klabu nchini Morroco,kama itakuwa Dili kamili inakuwa na mara nyingine tena Kwa Ngoma kucheza hapo kabla ya hapo aliwahi kucheza Raja Casablanca.
-1288233617.jpg
 
Anacheza slow sana akiwa na Kagoma pale kati mtaendelea kutawaliwa sana hata na Timu za kawaida Yanga walijaza viungo kama ugomvi aisee ikabidi Mpanzu nae awe anafata mipira kati maana akikaa kwa Mwenda wahuni hawapeleki mipira na ikipelekwa Mwenda anakua mtu wa kwanza kuuchukua..
 
Ngoma amepanic mno, makombe yamemkataa, pia hajui kuwa timu nzima ya Simba ni mdebwedo, ni underdog, badala yake hasira za kufungwa huwa anahamishia kwa Camara, inakera sana na lazima Ngoma akemewe asilete ubabe kwenye nchi yetu, tena mbele ya Camera zetu, ni ajabu kabisa nyie wachezaji mapro mnaojiona mnajua boli wote mmepitwa na sasa Pacome yuko uso kwa uso na Camara ambae ametoka kujaribu kuokoa ila Pacome ni mjanja mno, ni mtu na nusu, sasa Ngoma usie na akili ulitaka Camara afanyeje wakati we unalamba mchanga baada ya kushindwa kumkaba Pacome ukaenda chini na kutambaa kama mtoto? Kule Zenji pia Ngoma mpira ulimshinda kwa hasira alimsukuma sana Camara akidhani ndio tatizo kumbe tatizo ni yeye kushindwa kumudu katikati, this is bullying to Camara and unacceptable, nyie makolo huko mnakoomboleza kipigo cha paka shume, kipigo cha kumkoma nyani giladi, kipigo cha rungu linalotua kwa ndege anaekula mpunga , makolo mnaolia lia baada ya kupigwa kwa mara ya Tano hebu tokeni mafichoni, mkemeeni sana Ngoma aache bullying kwakuwa anampotezea Camara focus ya mchezo na kuharibu saikolojia ya timu nzima!

Anyway, baada ya kumponda sana Ngoma Sasa narudi kwenye Mada, Ngoma anacheza slow sana and not aggressive like Aucho ambae alitoka mbali na kuja kumtoa Mpanzu kwenye reli baada ya Mpanzu kuonesha makali yake kwa kuondoka na kijiji. Mpira wa nguvu na kusukumana Ngoma hautaki tena na ndio mpira unaochezwa bongo na duniani kwasasa. Ngoma hataki kuguswa, hataki kuchafuka jezi, hataki kuumizwa, kajaa ubishoo na kwa maana hiyo Simba itaendelea kupigwa bakora na Yanga tu, hebu mlinganishe Ngoma na Aucho au Duke Abuya au Mudathir, utaona how serious uto players are. Ngoma anatakiwa aende arabuni haraka , huko atacheza vizuri sana taratibu , kamanyola bila jasho. 😂
 
Back
Top Bottom