Kiungo wa Yanga Papy Kabamba Shishimbi atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari

Kiungo wa Yanga Papy Kabamba Shishimbi atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
OKWI TSHISHI.jpg

Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa Kamati ya Tuzo imemtangaza kiungo wa kimataifa wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu kwa mwezi Februari.

Tshishimbi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu yake ya Yanga, kuchukua alama 12 zote katika michezo minne iliyopigwa ndani ya mwezi Februari akifunga mabao matatu na kusaidia bao moja.

Tshishimbi amewaacha wapinzani wake kwenye kinyang'anyiro hicho ambao ni kiungo mwenzake wa Yanga Pius Buswita, aliyefunga mabao mawili pamoja na mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi aliyefunga mabao 4 na kuisaidia Simba kupata alama 10 katika mechi 4.

Nyota huyo raia wa DR Congo atakabidhiwa zawadi zake ikiwemo zawadi kubwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi kuu pamoja na tuzo ambayo imetambulishwa msimu huu na TFF.

Chanzo: EATV
 
Bora wampe Hako ka Million maana kwa mtani Hali ngumu tangu Kanjibhai ajitoe
 
Back
Top Bottom