Kiungulia kinanisumbua

Kiungulia kinanisumbua

napenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
485
Reaction score
90
Habari ya muda huu wanajukwaa.

Nina tatizo la kiungulia, kinanisumbua sana, sasa kina muda mrefu, yaani leo kipo kesho hakipo au kinafululiza. Mara nyingi kinakuja usiku muda wa kulala, kinasababishwa na nini? Tiba yake ni nini?

Asante.
 
Ni dalili ya vidonda vya tumbo
 
USICHOKIJUWA KUHUSU MARADHI YA KIUNGULIA






Kiingulia ni acidity iliyozidi kufuatia kula kitu chenye acidity. Maharage yakilala yana ferment hivyo kutengeneza more acidity state hivyo ukiyala vimengenyo vya pelipeptaid, peptaid na pepton vyenye kazi ya kuyeyusha wanga vinatoa acid nyingi ukichanganya na ile ya maharage matokeo yake ni kiungulia.

Dawa ya kiungulia ni kunywa alcalinine yoyote au base ili kuineutralize ile acid na kutengeneza chumvi na maji hivyo kutokuwa na madhara tena.

Dawa ya kawaida sana ni vidonge vya magnesium tricilicate au actal. Majivu yakichanganyika na maji yanatengeneza alcaline solution ambayo pia inaneutralize ile acid. Tatizo la majivu hakuna kipimo sahihi ukizidisha, hata ile acid ya kawaida ya kusaga chakula inakuwa neutralized hivyo chakula kinashuka kilivyo.

Usipotafuta suluhisho la kudumu kuicontrol hiyo acid tumboni kwako, inaweza kumungunya mpaka ngozi laini ta tumboni hivyo kusababisha vidonda vya tumbo vinaitwa ulcers.

DAWA YA KUTIBU KIUNGULIA KWA TIBA MBADALA:

KIUNGULIA::

TIBA;:

Changanya glasi moja (250ml) ya maziwa na kijiko kikubwa 10ml) cha mafuta ya habat soda.
Kunywa mchanganyiko huu na urudie kutwa mara tatu (1×3) kwa muda wa siku 5. tumia kisha uje unipe feedback chanzo.
USICHOKIJUWA KUHUSU MARADHI YA KIUNGULIA

Nigella_sativa_oil.jpg

 
Haya mafuta ya Habat Soda hapa Dar MziziMkavu tunayapata wapi!na baada ya kutumia huo mchanganyiko nitapona kabisa au ni dawa ya kutuliza?
 
Last edited by a moderator:
Haya mafuta ya Habat Soda hapa Dar MziziMkavu tunayapata wapi!na baada ya kutumia huo mchanganyiko nitapona kabisa au ni dawa ya kutuliza?
Nigella Sativa oil au Black seed Oil ;Mafuta ya Habat Soda yanapatikana mjini Dar kwenye Maduka ya wauza Dawa za Kienyeji Karibu na sokoni Kariakoo..............Kaulize utapata huko.Au Uliza kwenya Ma-Super Market Makubwa yaliyopo mjini Dares-Salaam Mkuu@stephot Dawa zangu mimi nikitoa ukitumia vile nitakavyo kuambia utapona kabisa sibahatishi dawa zangu nikikupa ujuwe ni dawa ya uhakika.
 
MziziMkavu Umenishauri vizuri, kama uliyvo sema ninatabia ya kupika maharage na kuyatumia siku mbili, hapo ndo kiungulia hunisumbua. nilikua sijui kama maharage yakilala ni sumu, kwa sababu kiungulia hunisumbua masaa kazaa usiku baada ya kutumia chakula na baadaye kinapotea, kuna haja ya kutumia dawa kwa siku tano? na je mwanza naipataje?
 
Last edited by a moderator:
Nimekupata mkuu,vipi hayo maziwa yanatakiwa yawe katika hali gani,moto au baridi?
 
Pia ukilamba majivu ya mkaa kiungulia kinakata hapohapo sema sio dawa ya kudumu, ni pale tu unapojisikia kiungulia
 
MziziMkavu Umenishauri vizuri, kama uliyvo sema ninatabia ya kupika maharage na kuyatumia siku mbili, hapo ndo kiungulia hunisumbua. nilikua sijui kama maharage yakilala ni sumu, kwa sababu kiungulia hunisumbua masaa kazaa usiku baada ya kutumia chakula na baadaye kinapotea, kuna haja ya kutumia dawa kwa siku tano? na je mwanza naipataje?
Mwanza tafuta kwenye maduka ya Dawa za kisuna uliza ukikosa nitafute kwa wakati wako mimi ninaye wakala wangu yupo hapo mjini Dar utampatia pesa yako atakununulia hayo Mafuta ya Habbat sawda .
 
Back
Top Bottom