Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mabadiliko makubwa ya mfumo wa homoni pamoja na kasi ya ukuaji wa mtoto ambayo huleta mgandamizo kwenye tumbo la chakula ni mambo mawili yanayosababisha kutokea kwa tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito.
Jambo hili siyo la ajabu, linaweza kutokea kwa mwanamke yeyote.
Ili kuzuia, kukabiliana pamoja na kupunguza changamoto zinazoambatana na tatizo hili, mambo yafuatayo yanashauriwa-
Chanzo: STG NEMLIT 2021
Jambo hili siyo la ajabu, linaweza kutokea kwa mwanamke yeyote.
Ili kuzuia, kukabiliana pamoja na kupunguza changamoto zinazoambatana na tatizo hili, mambo yafuatayo yanashauriwa-
- Kupunguza ulaji wa vyakula na vinywaji vinavyoongeza uzalishwaji wa asidi tumboni mfano pilipili, energy drinks na vyakula vyenye mafuta mengi.
- Kutokutumia kabisa pombe na sigara
- Kuepuka ulaji wa chakula kingi kwa mkupuo mmoja, badala yake kula chakula kidogo kila mara kwa kadri unavyoweza
- Kunywa maji mengi kila mara
- Epuka ulaji wa chakula cha usiku muda mchache kabla ya kwenda kulala, unashauriwa kula walau saa 2-3 kabla ya muda sahihi wa kulala
- Inua kidogo kitanda chako usawa wa kifua kwa kutumia mto au kitu chochote kile ili kuruhusu kifua kuwa juu zaidi kuliko sehemu ya chini ya mwili.
Chanzo: STG NEMLIT 2021