Nina tatizo kama hilo na nilichukulia ni maumivu ya kawaida, nikawa natumia dawa za kupunguza maumivu lakini hazikuwa na msaada niliamua kwenda hospital ambako nilipigwa X-RAY,bahati nzuri sikuwa na tatizo kubwa nikaandikiwa dawa aina mbili nazo ni ARCOXIA (etoricoxib,MSD) 90mg natumia kidonge kimoja katika masaa 24 na NORGESIC (450+35)mg kidonge kimoja kila baada ya masaa nane na kwa kweli nimepata nafuu sana kwa kuwa maumivu nilikuwa nayasikia mpaka miguuni..
Pili kuna mtu wangu wa karibu ana tatizo kama hili yeye kwa bahati mbaya X-RAY imeonyesha kuna mfupa umesogea kutoka mahala pake lakini alianza na dawa kama za kwangu lakini maumivu hayakumuondokea na aliporudi hospital ametakiwa afanyiwe tiba zaidi na ikishindikana itabidi afanyiwe upasuaji.
Ushauri wangu ni kama alivyo tanguliza MZIZI MKAVU mwambie muhusika aende hospital ndio uamuzi wa busara.