WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 456
Watu wengi wanashangaa na kushtushwa na mtifuano wa uchaguzi wa viongozi wa kitaifa ndani ya CHADEMA. Wanaona ni jambo jipya. Wengi wameanza na kubashiri chama kupasuka. Lakini ukweli ni kwamba kwa wafuatiliaji na watafiti wa siasa za upinzani hususan zinazohusu CHADEMA na chaguzi zake karibu zote za ndani hili si jambo jipya. Ingawa kuna tofauti za msingi ambazo lazima zitazamwe sasa kuliko wakati wowote ule vinginevyo kama si sasa basi wakati mfupi ujao kuna msiba.
Kwa miaka yote uchaguzi wa CHADEMA umekuwa ukibeba mshindo mkuu. Ukianzia uchaguzi ambao Chacha Wangwe (marehemu) alivaana na Mbowe, Zitto vs Mbowe na Sumaye vs Mbowe, chaguzi zote zilifanyika kwa vishindo vingi tu vikiacha mwangwi mkubwa lakini chama kikibaki thabiti. Sababu kuu za hili ni tatu au nne. Mosi, ni ushawishi na ukubwa wa chama chenyewe. Pili; ni oganaizesheni yake na kuwa na wanasiasa wenye kupendwa, washawishi, regenerative na wenye kushikamana, tatu; ni kuwa na kada ya wanachama vijana ambao wana utawala (dominance) wa mitandao ya kijamii na nne; ni nguvu za nje ambazo zimekuwa na maslahi yote mema na mabaya dhidi ya CHADEMA.
Kwa mwenendo wa uchaguzi wa mwaka huu, sababu ya pili, tatu na nne hapo juu zimekuwa na mabadiliko makubwa. Na hapa ndipo kuna mtego na kiunzi. Kwa miaka mingi kulikuwa na distinction na selective exposure kati ya CHADEMA kama taasisi, viongozi waandamizi na wanachama wake dhidi ya “watu wa nje” (hapa nisitumie wanaharakati maana kuna wenye kufanya kazi yao kweli lakini wengine kama Maria Sarungi, ni typical set up)katika kuendesha siasa zake. Lilipokuwa likija suala la chama chao, ulinzi ulikuwa mkubwa. Wanachama kote mitandaoni walikihami na kukitetea. Kauli zao zilikuwa thabiti kuanzia chini hadi juu.
Mtego na kiunzi kilianza na kufutwa au tuseme kuchorwa mstari mwembamba sana kati ya chama cha siasa, marengo, matarajio, mikakati, itifaki na uendeshaji siasa zake na msukumo wa kikundi cha nje (“wanaharakati” kwa tahadhari kubwa). Ieleweke kwamba hawa “wanaharakati” miaka yote wamekuwa na mrengo na muono hasi kwa chaguzi za CHADEMA. Walikwama kufanikiwa kwa sababu ya namba tatu hapo juu, ya kada ya wanachama vijana wa CHADEMA ambao wana utawala wa mitandao ya kijamii. Lakini pili, viongozi hao waandamizi walikuwa reserved wakikeep political distinction.
Maria Sarungi (ninamtaja kwa kurudia rudia) ndiye hasa amefanya kazi hiyo ya kufuta mstari huo au kuufanya uwe mwembamba sana sambamba na wana mkakati wa mitandaoni hususan club house. Kwanza; kimkakati ameingia katika kundi hilo la vijana wa Chadema, ambao kimsingi kutokana na kujikita katika siasa pekee, masoko ya ajira yamekuwa magumu kwao. Yamewatupa kutokana na mirengo yao. Hapa karibu wote walionaye hufanya anachowaelekeza na hawawezi hata nukta kwenda kinyume naye. Kimsingi, amejenga taasisi yake thabiti ndani ya vijana hawa wa CHADEMA.
Pili; ametumia vema fursa ya political oppression and shrinking of space kuwateka viongozi hao waandamizi wa CHADEMA ambao hupenda kuzungumza wakitegemea ndiyo namna ya kumaintain relevance. Wengi wamekuwa wakijipanga katika platform yake (na ile ya Club house kwa Tundu Lisu na timu yenye nusa nusa mtupu). Humo kimsingi huchimbwa na kufunguka kila kitu. Basically kwa mtu kama Tundu Lisu amefikia hatua ya kukiweka chama na mwenendo wake wa kitaasisi wazi. Huzungumza mambo kama msemaji wa mwisho wa taasisi na hata mara nyingine kutoa misimamo ya mambo ambayo yanakuwa yenajiri yenye kuathiri mwenendo wa national agenda and politics bila kusubiri chama chake kinasimama wapi. Ingawa ni haki yake kikatiba hii hutoa mwanya wa political divergence. Na kumfanya muda wote kusimama peke yake dhidi ya Chama chake. This was also similar to Peter Msigwa and ultimately his exit to the party.
Hali ni ileile kwa Maria Spaces na msururu wa makada waandamizi hao wa CHADEMA kupanga foleni kwake. Ukichanganya na kuteka kundi la compromised younger generation ya CHADEMA, amejenga informal institution ndani ya CHADEMA ambayo inaishi chini ya doctrines zake, kwani kutofautiana naye ni kupoteza ugali mezani. Na kwa viongozi waandamizi wamejenga nira kwake, kwa kujua au kutojua ambayo huwafanya wawe mateka na kushindwa kutofautiana naye wazi. Na mara kadhaa she seems demanding sort of pay back or loyalty. Hapa ndipo penye kiunzi na ndicho ikabidi kirukwe sasa kabla ya kuchelewa zaidi. Kuendelea hata kwa nukta moja kumtaasisisha Maria Sarungi ndani ya taasisi ya CHADEMA na kuwapa sikio wasiotaka kujoin party line huku wa kuonesha “kukipenda sana” ndiyo kuzidi kuteguka na kukwama kwenye kiunzi. Kuambatanisha malengo ya mwanaharakati na mwanasiasa, kwamba mwanasiasa afanye full committed kazi ya mwanaharakati huku mwanaharakati mwenyewe akiwa amekaa pembeni tena mbaya zaidi muda wote. Ni tatizo. Kiunzi kirukwe sasa.