Kivinje

Kivinje

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Haya wadau wa ujasiriamali na biashara,

Kuna hii biashara ya dagaa Kivinje, imepamba moto sana sasa hivi. Kinachoshangaza ni kwamba wanaopiga hela kubwa ktk biashara hiyo pale kivinje ni Wakongo. Hawa jamaa wamebadirisha kabisa hii biashara kwa kuongeza ubora wa dagaa hawa.

Dagaa wakivuliwa, wanachemshwa na maji ya kawaida, kisha wanaweka na chumvi kidogo na viungo fulani kisha wanawaanika ktk vichanja maalum. Dagaa likitoka hapo halitoi halufu kabisa na linakuwa tayari kuliwa.

Hawa jamaa wamefunika biashara nzima, jamaa wana mwaga hela vibaya, kisha wanasafirisha kupeleka huko wanakopeleka. Pia jamaa zetu toka Kigoma wapo pia.

Kwa nini kila eneo tunapigwa bao? hadi dagaa!!!!!!. Nauli toka Dar mpaka Kivinje ni Tsh 11,000/ kama unataka kwenda kujionea utajiri wa Kivinje, hasa hili dagaa linalopelekwa nje ya nchi. Hii fursa bado iko wazi, njooni muibe ujanja wa kuandaa dagaa, tusiandae dagaa kizamani.
 
Mkuu Malila hivi wewe hii nchi umezunguka yote eehe! unazungukaga kutafuta fursa, kujifunza au unakuwa kwenye business nazo? am just curious sir!
 
Back
Top Bottom